Ruka hadi kwenye maudhui makuu

MSIBA WA NGWAIR SASA UPO MBEZI BEACH

WAKATI rafiki wa msanii Albert Mangwea, M To The P naye amefariki dunia asubuhi ya leo nchini Afrika Kusini, familia ya marehemu tayari imeanza taratibu za mazishi.

Nyota wa Bongo Fleva, Albert Mangwea maarufu kama Ngwair, alifariki dunia jana jioni akiwa nchini Afrika Kusini.
Inadaiwa Ngwair alifariki dunia kutokana na kuzidiwa na matumizi ya dawa za kulevya na wakati mwili wake unakimbizwa hospitali ya St Hellen Joseph, rafiki yake naye, msanii pia M To Te P alikuwa katika hali mbaya, pia kwa utumiaji wa dawa za kulevya.
Taarifa kutoka Afrika Kusini, zimesema swahiba huyo wa Ngwair naye amefariki dunia.
Kaka wa marehemu Ngwair, Kenneth Mangwea amesema msiba upo Mbezi Beach, Goigi mjini Dar es Salaam na taratibu za kuirejesha miili ya marehemu nyumbani zimeanza.
Tayari vifo vya wasanii hao wawili vimeanza kuzalisha maswali magumu, kubwa likiwa ni utumiaji wa dawa za kulevya pekee ndio umesababisha vifo vyao, au kuna mambo yaliyojificha.   
Kimuziki, Ngwair aliibukia mkoani Dodoma ambako alikuwa katika kundi moja na Dark Master, Noorah na Mez B na amekuwa akishirikiana na M To The P tangu akiwa msanii anayechipukia baada ya kuhamia Dar es Salaam.
Baada ya kuja Dar es Salaam, Ngwair akapata dili Bongo Records chini ya mmiliki wa studio hizo, Petter Matthysse ‘P Funk’ aliyemuinua zaidi kimuziki na kumfanya awe miongoni mwa wanamuziki nyota nchini.
Wimbo wake wa kwanza kutamba ni Gheto Langu mwaka 2003 ambao ulimpatia umaarufu kabla ya kutoa albamu yake ya kwanza a.k.a Mimi mwaka 2003 ambayo ilimpatia mafanikio makubwa na kubadili maisha yake.
Hata hivyo, mafanikio hayo yalimlevya na kujitumbukiza kwenye utumiaji wa dawa za kulevya, hivyo kujikuta akishindwa kufanya kazi ya muziki kwa usanifu na kuanza taratibu kufilisika hadi kuuza mali zake zote, ikiwemo gari aina ya Jeep.
Ngwair kutoka kwenye kupanga nyumba nzima maeneo ya Sinza, Dar es Salaam akajikuta anarejea kuishi katika ‘magheto’ ya washkaji zake sehemu mbalimbali Dar es Salaam.
Mwaka 2010, Athumani Tippo, mmiliki wa maduka ya Zizzou Fashions alijaribu kumuinua tena msanii huyo baada ya kumchukua kwenye lebo yake na kumuwezesha kutoa albamu ya pili, Nge.
Hata hivyo, Nge haikufanya vizuri sana na kuzidi kumchanganya msanii huyo hivyo kutopea kwenye dimbwi la utumiaji wa dawa za kulevya na ‘kuharibika zaidi’.  
Mafanikio yake zaidi ni kushinda tuzo ya Kilimanjaro Music Awards kama mwana Hip Hop Bora wa mwaka 2005. 
Mwaka 2003, msanii Wayne Wonder aliyekuja kutumbuiza kwenye Fiesta aliondoka na CD ya wimbo Mikasi ya Ngwair baada ya kuvutiwa na kibao hicho alichowashirikisha Mchizi Mox na Ferooz. 
Ngwair alijaribu sana kumuinua kimuziki M, lakini pamoja na ukweli kwamba alikuwa ana kipaji, lakini hakufanikiwa, ingawa aliwahi kutoa albamu.
Pumzikeni kwa amani. Mbele yenu, nyuma yetu. RIP.

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

FIFA yatoa orodha ya vilabu bora duniani, Simba na Yanga zachuana vikali

SHIRIKISHO la Soka Afrika (CAF) limetoa orodha ya viwango vya ubora wa klabu barani, Simba ikiendelea kuwa juu ya klabu nyingine za Tanzania, nafasi ya tano. Orodha hiyo imetoka leo kuelekea droo ya hatua za awali za michuano ya klabu Afrika ambayo kwa mara ya kwanza kihistoria itafanyika nchini katika studio za Azam Tv, Tabata Jijini Dar es Salaam. Yanga ambayo kama Simba itashiriki Ligi ya Mabingwa — yenyewe inashika nafasi ya 12, wakati timu nyingine katika orodha hiyo ni Namungo FC wanaoshika nafasi ya mwisho, ya 75 kwa pamoja na Salitas FC ya Burkina Faso, Ahli Benghazi ya Libya na NAPSA Stars ya Zambia. Kwa msimu ujao mbali na Simba na Yanga kushiriki Ligi ya Mabingwa, Azam FC na Singida Black Stars zitashiriki michuano ya Kombe la Shirikisho Afrika.

HISTORIA YA TIMU YA MASHUJAA YA KIGOMA, KUMBE NI SHEA YA JESHI NA WANANCHI

Timu inaitwa Mashujaa Lake Tanganyika FC ( Mashujaa FC ) ilianza rasmi kampeni yake ya kupanda Ligi Kuu tarehe 29/9/2018 na imepanda Ligi Kuu 25/06/2023 miaka mitano ya kupambana kwenye Ligi Daraja la kwanza Championship. Timu hii inaendeshwa kwa ushirikiano wa pande mbili kati ya Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) na Halmashauri ya Manispaa ya Kigoma Ujiji kwa niaba ya Wananchi wa Kigoma. Muelewe hapa maana wengi wanasema ni timu ya Jeshi asilimia 100% Nembo ya timu ni Sokwe Dume, Shujaa wa Hifadhi za Gombe na Mahale zilizopo mkoani Kigoma. Rangi ya kwanza ya jezi ya timu (first kit) ni hiyo hapo chini na kwenye nembo ya timu ni rangi za tunda la michikichi (mawese ). Hii kama njano ni mawese yaliyoganda na huo wekundu ni mawese ya moto. Ukishika tunda la Mse juu utaona wekundu na ukikata katikati utaona njano. Nyeupe ni ‘nazi’ ya Mse hizi ni alama za utajiri wa Kigoma Jezi nyingine ni blue inayowakilisha Ziwa Tanganyika na Jezi nyingine ni Nyeupe

Beno Ngassa mdogo wa Mrisho Ngassa anayekipiga Tanzania Prisons

Miongoni mwa viungo wa pembeni wanaofanya vizuri ni Benodict Khalfan Ngassa ambaye amekuwa akifanya vizuri. Ngassa ambaye ni mtoto wa mchezaji wa zamani wa Pamba Jiji na Simba SC, Khalfan Ngassa, pia ni mdogo wa kiungo mshambuliaji wa zamani wa Yanga, Simba na Azam, Mrisho Ngassa anatajwa ni mmoja kati ya wachezaji wanaotazamiwa kufanya makubwa siku za usoni. Mambo Uwanjani Blog itawaletea Makala maalum ya kiungo huyo hatari ambaye ndoto zake ni kufuata nyayo za kaka yake Mrisho Ngassa. Beno Ngassa