MONACO SASA WATISHA DUNIA...WAVAMIA DARAJAN
BEKI Branislav Ivanovic anatakiwa na Monaco baada ya kumkosa Vincent Kompany kutoka Manchester City.
Mlinzi huyo mwenye umri wa miaka 29 wa
Chelsea amependekezwa na kocha Claudio Ranieri kwa mmiliki bilionea wa
Kirusi, Dmitry Rybolovlev katika mpango wa kuijenga timu hiyo iliyopanda
Ligi Kuu Ufaransa iwe tishio.
Walitoa oda ya Pauni Milioni 51.3
iliyokubaliwa na Atletico Madrid kwa mshambuliaji Radamel Falcao, ambaye
anatarajiwa kufanyiwa vipimo leo, baada ya Ijumaa kukamilisha mpango wa
kuwasajili kwa Pauni Milioni 60 wachezaji wawili wa Porto, Joao
Moutinho na James Rodriguez.
Monaco ipo tayari kutoa kiasi cha Pauni
Milioni 25 kumnasa Ivanovic, ambaye alifunga bao la ushindi katika
fainali ya Europa League, lakini pia anatakiwa na kocha mpya wa Chelsea,
Jose Mourinho.
'Special One' alijaribu kumsajili
Ivanovic msimu uliopita akiwa bado Real Madrid lakini akakwama baada ya
Chelsea kupandisha bei yake, na atataka Mserbia huyo aendelee kuwa
sehemu ya kikosi cha msimu ujao.
Pamoja na hayo atapenda kumsajili
Raphael Varane wa Real Madrid na beki ambaye Mourinho anaweza kumuacha
ni David Luiz, ambaye anatakiwa na Barcelona.
Monaco pia inamtaka Hatem Ben Arfa wa Newcastle.