ARSENAL SASA WAINYIMA RAHA KABISA MAN UNITED KATIKA DILI LA FABREGAS
KLABU
ya Manchester United inaweza kulazimika kutoa fedha nyingi ili kumpata
Cesc Fabregas, kutokana na Barcelona kuwa tayari kuwauzia mchezaji huyo
Arsenal kwa nusu bei kulingana na makubaliano yao wakati anahamia Nou
Camp.
Inamaanisha Barcelona ingeweza kumuuza kwa Pauni Milioni 70 mchezaji huyo, lakini The Gunners wanaweza kupewa ofa ya kumsajili kwa Pauni Milioni 20, hivyo United lazima wapande dau.
United
ina nia thabitio ya kumsajili kiungo huyo wa Hispania, lakini Arsenal
sasa ndio imeshikilia mustakabali wa dili hilo na ndiyo wataamua kama
kocha mpya David Moyes atampata nyota huyo au la.
Ilikubaliwa wakati Fabregas anarejea Catalan mwaka 2011, kwamba The Gunners watapunguziwa asilimia 50 akiuzwa.