MTANZANIA AZIDI KUTESA ULAYA
KIUNGO
chipukizi Mtanzania, Adam Nditi jana aliendelea kuwa nje wakati timu
yake, Chelsea ilipolala 1-0 mbele ya Norwich ugenini, bao pekee la
Cameron McGeehan dakika ya mwisho kwa penalti katika Fainali ya kwanza
ya Kombe la FA la Vijana.
Mechi ilionekana itaisha kwa sare hadi
beki wa Chelsea, Alex Davey alipodaiwa na refa Neil Swarbrick
kumuangusha kwenye eneo la hatari Joshua Murphy katika dakika ya pili ya
dakika za nyongeza.
McGeehan hakuiangusha beji yake ya
Unahodha na akaenda kuukiwamisha nyavuni mkwaju wa penalti akimtungua
kipa Mitchell Beeney na kuwainia kwa shangwe mashabiki wa nyumbani,
Uwanja wa Carrow Road ambao walikuwa zaidi ya 22,000.
Chelsea ilitawala mchezo huo na
kutengeneza nafasi nzuri, ambazo walishindwa kuzitumia, lakini waapewa
nafasi kubwa ya kuupiku ushindi huo mwembamba katika mchezo wa marudiano
nyumbani, Uwanja wa Stamford Bridge wiki ijayo.
Sasa ni mwezi wa pili, Nditi anayetokea
visiwani Zanzibar anakosekana kabisa katika kikosi cha Chelsea, hata
benchi hakai na haijulikani nini kinachomsibu kama ni majeruhi au
amepokonywa namba.
Lakini BIN ZUBEIRY itaendelea
kufuatilia ili kujua ukweli juu ya kiungo huyo aliyebeba matumaini ya
Watanzania wengi kwamba ataling'arisha jina la nchi yake katika klabu
kubwa Ulaya.
Kikosi cha Norwich City kilikuwa: Britt, Norman, Wyatt, McGeehan, McFadden, Toffolo, Murphy, Randall, Morris, King/Young na Murphy.
Chelsea: Beeney, Aina, Davey, Ake, Wright, Baker, Kiwomya, Loftus-Cheek, Feruz/Musonda, Colkett/Swift na Boga
La ushindi jioni: Nahodha wa Norwich, Cameron McGeehan akifunga kwa penalti. Chini anapongezwa na wenzake.