Said Ndemla aibukia Kagera Sugar

Wana Super Nkurukumbi, Kagera Sugar FC wamemtambulisha kiungo wa zamani wa Simba SC, Saidi Hamisi Ndemla kama mchezaji mpya klabuni hapo kwa uhamisho huru baada mkataba wake na JKT Tanzania kufikia ukomo.

Kiungo huyo wa kati mwenye umri wa miaka 30, raia wa Tanzania anatua kwenye klabu hiyo iliyopanda daraja l kwenda Ligi Kuu Bara kwa msimu wa 2026-2027 ikiwa ni muendelezo wa maboresho ya kikosi hicho.