Yanga na Simba kuanzia ugenini Ligi Kuu bara
VIGOGO wote, Simba na Yanga wataanzia ugenini msimu mpya wa Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara dhidi ya timu za Namungo FC na Kagera Sugar katikati ya mwezi ujao.
Wakati mabingwa watetezi, Yanga SC watakuwa Uwanja wa Majaliwa, Ruangwa mkoani Lindi dhidi ya wenyeji, Namungo FC Agosti 15, watani wao na washindi wa pili wa msimu uliopita, Simba SC watakuwa Uwanja wa Kaitaba, Bukoba dhidi ya wenyeji, Kagera Sugar siku itakayofuata Agosti 16.














