Simba yashikws shati na Mogadishu
Wawakilishi wa Tanzania bara katika michusno ya Kagame Cup, Simba usiku huu wameanza vibaya baada ya kutoka sare ya 0-0 na timu ya Mogadishu City Club ya Somalia.
Mashindano hayo yanafanyika nchini Rwanda na kudhaminiwa na klabu ya Al Hilal ya Sudan, tumeshuhudia Simba na Mogadishu wakicheza soka zuri na lenye ufundi.
Almanusura Simba ipate bao dakika za mwisho mwisho kupitia mshambuliaji wake mpya Ibrahim Doumbia baada ya kugongesha mwamba.
Katika mchezo mwingine wa kundi hilo, Jamus SC kutoka Sudan Kusini imeilaza Singida Black Stars kwa mabao 2-0 na kushika usukani wa kundi hilo.
