Simba yaonesha jeuri ya pesa, yagomea hoteli


Wakati vilabu vingine ambavyo vinashiriki michuano ya CECAFA Kagame Cup 2026 vikifikia kwenye hoteli ambazo zinalipiwa na CECAFA zenye hadhi ya nyota tatu.

Simba iliwajulisha CECAFA kwamba itafikia kwenye hoteli yenye hadhi ya juu zaidi na italipa gharama zote za ziada ili kuendana na hadhi na ukubwa wa klabu yao baada ya Raisi wa heshima wa klabu hiyo Mohammed Dewji kuagiza kwamba wanastahili kuhukua hotel ya hadhi ya nyota 5 na atalipia kila kitu yeye!

Hivyo Simba wamefikia hoteli ya nyota 5 ya Mövenpick yenye hadhi ya juu zaidi jijini Kigali ambayo Gharama ya chini ya chumba ambacho kinachotumiwa na staff wa Simba ni Tsh. 450,000 kwa siku moja ikihusisha chai ya asubuhi pekee. Simba wamesafiri na chakula chao kutoka Tanzania ambacho watatumia muda wote ambao kikosi kitakuwepo nchini Rwanda.

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

FIFA yatoa orodha ya vilabu bora duniani, Simba na Yanga zachuana vikali

Kocha Simba anataka wachezaji wapya watano

Beno Ngassa mdogo wa Mrisho Ngassa anayekipiga Tanzania Prisons