Peter Shalulile rasmi Yanga
Taarifa kuhusu uwezekano wa Peter Shalulile kujiunga na Young Africans SC (Yanga) zimezidi kushika kasi, huku mashabiki wa klabu hiyo wakianza kuhusisha dokezo lililotolewa na Meneja wa Habari na Mawasiliano wa Yanga, Ally Kamwe, kupitia ukurasa wake wa Instagram.
Ally Kamwe aliandika ujumbe wenye mafumbo, jambo lililoibua hisia na kuzua mjadala miongoni mwa mashabiki wa Wananchi, ambao baadhi yao wamehusisha ujumbe huo na nyota huyo wa Namibia.
Shalulile, ambaye ametengeneza jina kubwa akiwa na Mamelodi Sundowns, kwa sasa ni mchezaji huru baada ya kumaliza mkataba wake na klabu hiyo.
Yanga inaendelea na harakati za kuimarisha kikosi chake kuelekea msimu mpya, huku ikijiandaa kwa mashindano mbalimbali, ikiwemo CAF Champions League.Endapo usajili wa Shalulile utathibitishwa, atakuwa mmoja wa washambuliaji wenye uzoefu mkubwa wanaoweza kuongeza nguvu kwenye safu ya ushambuliaji ya Wananchi.
