Neo Maema mguu pande Simba
Kiungo Neo Maema bado hajafikia makubaliano na Simba SC ya kuongeza mkataba mpya ili kuendelea kuitumikia klabu hiyo kwa msimu ujao baada ya mkataba wake kumalizika!
Neo Maema anahitaji mshahara mkubwa ili kubaki Simba SC na hilo ndio jambo linaloleta ugumu sana kuweza kupewa mkataba wa muda mrefu,na Simba SC bado wanamuhitaji Neo Maema abaki kutokana na uzoefu wake kwenye Klabu Bingwa Afrika.
Bado mazungumzo yanaendelea baina ya pande zote mbili ili kufikia muafaka wa mwisho kama atabaki Msimbazi au ataondoka mapema sana na kabla ya msimu wa 2025-26 haujamalizika Neo Maema tayari alikuwa na machaguo yake kwa klabu za Afrika Kusini
