Hassan Mubiru atambulishwa Azam FC
KLABU ya Azam FC imemtambulisha winga wa kulia wa Kimataifa wa Uganda, Hassan Mubiru (21) kutoka SC Villa ya kwao, Kampala akiwa mchezaji mpya wa tano kuelekea msimu ujao.
Wengine ni mabeki wa kati, Lupini Mawuku Dieumerci (20) kutoka AS Maniema Union ya kwao, DRC na Henri Braham Stanic Mbelgiji mwenye asili ya DRC pia kutoka Stellenbosch FC ya Afrika Kusini.
Azam FC pia imesajili mawinga wengine wawili,, Henoc Molia (22) kutoka St. Eloi Lupopo ya kwao, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) na Muivory Coast, Kipré Tiagori Emmanuel Junior Zunon ‘Kipre Junior’ aliyejiunga tena na Azam FC akitokea MC Algiers ya Algeria.
Kipre Junior amerejea Azam FC ambako awali alicheza kuanzia msimu wa 2022-2023 akitokea SOL FC d’Abobo ya kwao, Ivory Coast hadi 2024-2025 alipohamia MC Algiers.
Hassan Mubiru
Azam Football Club
