HOZA ATOBOA SIRI YA MAKUNDI YA PANYA ROAD NA WAASI DAR ES SALAAM

Mdau wa michezo jijini Dar es Salaam  Prince Salum Hoza amesema wakati wake alipokuwa mratibu wa michuano ya soka kwa vijana chini ya miaka 20 Hozaboy cup kwenye uwanja wa shule ya msingi Tabata jijini makundi ya kihuni kama ya Panya road na waasi hayakuwepo.

Hoza aliyasema hayo akizungumza na mtandao huu ambapo amedai vijana wa kihuni walikuwepo tena wengi ila walishiriki ipasavyo kwenye soka.

'Zamani tuliandaa mashindano mengi ya soka nikishirikiana na mwalimu Kenny Mwaisabula 'mzazi', alisema Hoza ambaye kwa sasa ni mchambuzi katika gazeti la Msimbazi.

Hoza amewataka wadau wa soka jijini
kuanzisha michuano ya soka kwa vijana ili kupunguza uharifu na kusaidia kupatikana kwa ajira kwani mchezo huo umekuwa ukisaidia vijana mbalimbali kufanikiwa kimaisha kama akina Mbwana Samatta, Thomas Ulimwengu, Juma Kaseja, Mrisho Ngassa ambao wamefanikiwa kupitia soka

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

HISTORIA YA TIMU YA MASHUJAA YA KIGOMA, KUMBE NI SHEA YA JESHI NA WANANCHI

STAA WETU: JEREMIA JUMA MTOTO WA JUMA MGUNDA ALIYEIKACHA SIMBA NA KUENDELEA NA UASKARI

MAKALA: SIMBA NI TIMU YA KWANZA TANZANIA KUINGIA NUSU FAINALI AFRIKA