KERR MBISHI NA HASHAURIKI- MATOLA
Ilianza kama utani, lakini hatimaye juzi usiku ikawa kweli baada ya Kocha Msaidizi wa Klabu ya Simba, Selemani Matola kutangaza rasmi kutema kibarua hicho.
Matola, beki wa zamani wa klabu hiyo, amesema amefikia uamuzi huo baada ya kushindwa kuelewana na bosi wake, Kocha Mkuu, Dylan Kerr.
Akizungumza muda mfupi baada ya kujiondoa Simba usiku wa kuamkia jana, Matola alisema tabia ya ubishi na kutoshaurika kwa Kocha Kerr ndiyo sababu iliyom kimbiza Msimbazi.
Alisema uongozi wa Simba una taarifa za kuondoka kwake, kwani alifanya hivyo baada ya kikao kilichoongozwa na Rais wa Simba, Evans Aveva juzi usiku.
“Nimeamua kukaa pembeni, mambo yalikuwa yanazidi kuwa magumu, nilikutana na Evans tangu saa mbili usiku (juzi usiku), tumeongea lakini, msimamo wangu ulikuwa palepale,” alisema Matola, kiungo wa zamani wa RTC Kagera na Super Sport ya Afrika Kusini.
Aliongeza: “Msimamo wangu ni kujiondoa kabisa kufundisha Simba kwa sasa, sitaki hata kwenda timu B.”
Alisema mara kadhaa amekuwa akiripoti kwa uongozi kwa klabu kuhusu kutofautiana kwake na Kerr, lakini jambo la kushangaza hakuna suluhisho lolote lililofikiwa.
“Ratiba yake ya mazoezi hairidhishi kabisa, nilimweleza rais (Aveva) na alikuja kwa siri kwenye mazoezi na kushuhudia ukweli, lakini hakuna alilofanya hadi sasa,” alisema.
Alisema ni jambo la kushangaza kwa klabu kubwa kama Simba kufanya mazoezi mara moja kwa siku wakati inakabiliwa na mechi ngumu ligi kuu.
“Timu inapaswa kufanya mazoezi mara mbili kwa siku--asubuhi na jioni, lakini Kerr kwake siyo hivyo. Mazoezi ni asubuhi tu, ukimshauri kinyume inakuwa tabu,” alisema.
Kuhusu kiwango cha timu hiyo, alisema ni udhaifu kutokana na ukweli kwamba wachezaji wanapumzika muda mwingi badala ya kufanya mazoezi.
“Mazoezi ni muhimu sana kwa mchezaji na kadri anavyofanya mazoezi mara kwa mara ndivyo anavyojenga stamini na uwezo.
“Tulipokuwa Mbeya, nilishindwa kumvumilia alipobadili wachezaji saba katika kikosi kilichoshinda dhidi ya Mbeya City, akapanga timu yake na matokeo tulifungwa. Tuliporudi Dar niliueleza uongozi, lakini ukawa kimya hadi napotangaza kujiondoa,” alisema Matola.
Mkuu wa Idara ya Habari na Mawasiliano ya Simba, Haji Manara alisema uongozi utakutana katika kikao cha dharura kujadili hali ilivyo ndani ya klabu.
Matola alikuwa kocha wa vijana wa klabu hiyo tangu 2010 na baadaye kupandishwa cheo na kuwa Kocha Msaidizi kwa makocha Patrick Phiri (Zambia), Zdravko Logarusic (Croatia) na Goran Kopunovic (Serbia).
BAADA YA KUJIONDOA
Matola alisema kwa sasa yuko kwenye mazungumzo na klabu ya Bulyanhulu ya Shinyanga na wakiafikiana ataanza kuinoa timu hiyo inayocheza Ligi Daraja la Kwanza.