MAKALA: JUSTUCE MAJABVI: Kutoka Bundesliga hadi VPL


SI kazi rahisi kumnyang'anya namba Jonas Mkude mtoto wa 'Don Town', alishindwa Mrundi Pierre Kwizera aliyekuwa akicheza soka la kulipwa Ivory Coast, Mkude alimwachia nafasi wakati yeye akijiuguza majeraha yake ya goti, lakini alirejea kwenye nafasi yake baada ya Kwizera kushindwa kumshawishi kocha wa Simba wakati huo Mzambia Patrick Phiri.

Kwizera hakumridhisha kabisa kocha wa Simba Patrick Phiri ambaye aliamua kuachana naye na kuendelea kumtumia Mkude, Mkude anamudu kucheza namba sita na kwa kipindi kirefu hajatokea wa kumzidi.

Mwanzoni mwa msimu huu uongozi wa Simba uliamua kumsajili Mzimbabwe Justuce Majabvi aliyekuwa kicheza soka la kulipwa nchini Vietnam katika timu ya Vicem Hai Phong FC inayoshiriki ligi kuu nchini humo.

Ujio wake umechagizwa na kocha mkuu wa Simba Muingereza Dlan Kerr ambaye naye alikuwa akiifundisha timu hiyo, Kerr anamfahamu vizuri Majabvi na ndiyo maana akapendekeza asajiliwe haraka, lakini kocha huyo hakutambua kama Simba inaye kiungo matata Jonas Mkude.

Mkude si kiungo wa masihara, anajua nini anachokifanya, Majabvi naye si mchezaji wa kitoto kama wengi walivyodhana, ni mmoja kati ya wachezaji wa daraja la juu Zimbabwe, isipokuwa umri wake unaelekea kumtupa.


Anacheza namba sita kama Mkude, ingawa anaweza pia kucheza namba tano maarufu kama sentahafu, anacheza vizuri na kama ukibahatiksa kumtazama unaweza kuvutiwa naye, nyota huyo aliyewahi kucheza timu ya taifa ya Zimbabwe alizaliwa Machi 26, 1984 huko Harare.

Majabvi akimdhibti mchezaji wa timu pinzani, ligi ya Austria

Timu yake ya kwanza ilikuwa Lancashire Steel FC aliyoanza kuichezea mwaka 2002 hadi 2005 alipojiunga na Dynamo FC pia ya Zimbabwe, aliichezea timu hiyo kuanzia mwaka 2006 hadi 2008, msimu uliofuata wa 2009 alijiunga na Lask Linz ya Austria ambayo alidumu nayo hadi mwaka 2011.

Sifa za Majabvi zilianzia Zimbabwe ambapo alipokuwa anaichezea Dynamo aliiwezesha kufika nusu fainali ya ligi ya mabingwa Afrika, pia alipokuwa Austria katika klabu ya Lask Linz aliiwezesha timu yake kumaliza nafasi ya tatu katika ligi kuu ya nchini humo maarufu kama Bundesliga.

Majabvi aliihama Lask Linz na kujiunga na Khatoo Khan Hoa FC ya Vietnam kuanzia mwaka 2012 ambapo hakukaa sana kabla ya kujiunga na Vicem Hai Phong FC pia ya Vietnam aliyojiunga nayo mwaka 2013 hadi 2014, na mwaka huu amejiunga na Simba ya Tanzania.

Tayari Majabvi ameshaifungia goli moja Simba wakati ilipoifunga Mgambo Shooting 2-0 jijini Tanga, Majabvi anacheza vizuri kiasi kwamba kocha Dylan Kerr ameamua kumbadili namba Mkude na kumchezesha sentahafu au namba saba ili mradi kiungo huyo Mzimbabwe asimame katikati, Majabvi alimfunika vilivyo kiungo wa Yanga Mzimbabwe Thabani Kamusoko wakati miamba ya soka nchini Simba na Yanga zilipomenyana Septemba 26 mwaka huu, Huyo ndiyo Justuce Majabvi Mzimbabwe aliyetesa ligi ya Bundesliga na sasa anakipiga VPL

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

HISTORIA YA TIMU YA MASHUJAA YA KIGOMA, KUMBE NI SHEA YA JESHI NA WANANCHI

MAKALA: SIMBA NI TIMU YA KWANZA TANZANIA KUINGIA NUSU FAINALI AFRIKA

STAA WETU: JEREMIA JUMA MTOTO WA JUMA MGUNDA ALIYEIKACHA SIMBA NA KUENDELEA NA UASKARI