Taarifa za ndani kutoka jijini Mwanza ilipo kambi ya timu ya Pamba Jiji FC inayoshiriki Ligi Kuu bara, inasema kwamba uongozi wa timu hiyo umeingia mchecheto kuelekea mchezo wake dhidi ya Simba SC keshokutwa.
Mchezo huo utakaopigwa uwanja wa CCM Kirumba, uongozi wa timu hiyo umedai tangu timu yao ipande Ligi Kuu bara hawajawahi kuifunga Simba hivyo itakuwa ngumu kupata matokeo keshokutwa.
Hofu hiyo imekuja sasa kutokana na Simba kubadilika na kucheza soka la kuvutia kiasi kwamba hata wapinzani wao wakuu Yanga kurudi nyuma walipokutana nao hivi karibuni.
Lakini hata hivyo uongozi huo umewaambka mashabiki wa timu hiyo kutokana tamaa kwani lolote linaweza kutokea na wanaweza kuibuka na ushindi.
