Klabu ya Young Africans imetoa ripoti rasmi ya kitabibu inayowahusu wachezaji wake wanne ambao wameingia kwenye mkumbo wa majeraha, jambo linalozidi kutoa mtihani kwa benchi la ufundi la kocha Pedro Gonçalves.
Orodha ya Majeruhi na Muda wa Kukaa Nje:
Ibrahim Abdullah (Bacca): Beki huyu kisiki amepata jeraha la nyonga. Taarifa za kitabibu zinaeleza kuwa atakuwa nje ya uwanja kwa muda wa wiki tatu.
Laurindo Dilson (Depu): Mshambuliaji huyu amepata majeraha ya nyama za paja na atalazimika kukaa nje kwa kipindi cha wiki mbili.
Chadrack Boka: Beki wa kushoto amepata jeraha la enka (foot ankle) ya mguu wa kushoto, jambo litakalomuweka nje kwa wiki mbili.
Edmund John: Amepata jeraha la bega na atakuwa nje ya uwanja kwa muda wa wiki mbili.
Hali hii inaongeza presha kwenye kikosi cha Yanga ambacho tayari kinapambana na mapengo ya Dickson Job na Clement Mzize, huku ikilazimisha mabadiliko makubwa katika safu ya ulinzi na ushambuliaji kuelekea mechi zijazo za Ligi Kuu ya NBC.



