Inaandikwa na Fikiri Salum
Ilipoishia
Nabii Ismail hakuwa Mwarabu lakini baada ya kukaa hapo Makkah na kutifuka chemchem ya Zamzam, walikuja Waarabu wa Kiyemeni wa kabila la Qurhum na walipoona maji hapo waliomba kubakia hapo na ndipo Nabii Ismail akakulia kwenye kabila hilo na kujifunza Kiarabu na kuoa katika kabila hilo.
Endelea
MASKANI YA MWARABU YA ASILI
Waarabu kama tulivyoeleza hapo nyuma mwanzo walikuwa wakiishi Yemen lakini baadaye wakaanza kutawanyika kwenye sehemu nyinginezo za Bara Arabu, na Kwa kuwa wengi wao walikuwa wakiishi maisha ya kibedui ya kusafiri kutoka mahali pamoja kwenda kwingine kutafuta chakula na maji kwa nafsi zao na wanyama wao.
Waliweza kuenea sehemu zote za Bara Arabu na kufika Shamu na Iraq na Misri na Afrika mashariki na Afrika Kaskazini, kutawanyika huku kulizidi kwa kasi baada ya kuvunjika bwawa lao kubwa lililokuwa Maarib huko Yemen lililokuwa likilimbika maji mengi kwa ajili ya ukulima na mabustani yao na malisho ya wanyama wao.
Na mtawanyo mkubwa wa pili ni baada ya kuja Uislamu na kuhitaji kupeleka watu sehemu mbalimbali ulimwenguni kueneza dini hii.
Hapo ndipo Waarabu walipotawanyika kila mahali ulimwenguni kueneza neno la mwenyezi Mungu na kufikisha ujumbe wake, na ndiyo maana leo tunaona Waarabu katika bara na Manara ya ulimwengu.
ULIMWENGU WA WAARABU LEO
Waarabu leo wako kila mahali ulimwenguni, lakini kila ukikaribia kwenye kitovu cha dunia ambacho Kiko bara Arabu, Uarabu unazidi kudhihirika zaidi na lugha yao inazidi kuwa fasihi zaidi na hapa ndipo mila zao zinazidi kuifadhiwa na kutiliwa mkazo.
Aidha Waarabu wanaishi kwenye nchi zaidi ya ishirini za mashariki ya kati, ikiwemo bara Arabu na Shamu na Iraq na nchi za Ghuba ya Uajemi (Uarabu) na Afrika Kaskazini na mashariki, kuna ushirikiano katika jumuiya ya nchi za Kiarabu.
IDADI YA WAARABU LIMWENGUNI
Waarabu ulimwenguni wanahesabika kuwa idadi yao imefikia mia tatu milioni (180,000), ijapokuwa kuna idadi kubwa vile vile ya watu wa makabila mengine ambao wanaishi kwenye nchi za Kiarabu kama Mairani na Wahindi na Maarmani na Wayahudi, Mabarbari na Waafrika na Maburushi, Wakurdi na Waturuki na wengineo.
Kwa upande mwingine, kuna Waarabu wengi sana ambao wametawanyika katika nchi mbalimbali za dunia kwenye Manara yote ya ulimwengu...
INAENDELEA
