Uzinduzi wa Wiki ya Wananchi kufanyika Katoro
Klabu ya Young Africans SC imetangaza rasmi kuwa uzinduzi wa Wiki ya Mwananchi 2026 utafanyika Katoro, mkoani Geita, ikiwa ni sehemu ya maandalizi ya msimu mpya wa mashindano.
Akizungumza, Meneja wa Habari na Mawasiliano wa Yanga SC, Ally Kamwe, amesema klabu hiyo pia itazindua rasmi jezi mpya za msimu wa 2026/2027 mwishoni mwa mwezi huu.Uzinduzi huo unatarajiwa kuwakutanisha maelfu ya mashabiki wa Yanga kutoka maeneo mbalimbali ya nchi, huku ukiwa mwanzo wa maandalizi rasmi ya timu kuelekea msimu mpya wa Ligi Kuu ya NBC na mashindano ya kimataifa.
