Slavia Prague yabisha hodi Msimbazi
Klabu ya Slavia Prague,Czechia imetuma ofa kwenda Simba ili kumpata Hussein Ally Mbegu (16).
Slavia wanataka kinda huyo akafanye majaribio kwa siku kadhaa ili wajiridhishe na baadhi ya vitu kabla ya kulipa pesa Simba na kukamilisha manunuzi hayo.
Barua ya ofa iko Simba ila bado hawajajibu chochote.
