Simba yamnasa Kouasi
Simba SC inaendelea na harakati za kuimarisha kikosi chake huku beki wa kulia Blè Kouasi akitajwa kuwa kwenye rada za Wekundu wa Msimbazi.
Nyota huyo anasifiwa kwa uwezo wake wa kupanda na kushuka kwa kasi, pamoja na kupiga krosi zenye ubora mkubwa.
Endapo usajili huu utakamilika, ushindani katika nafasi ya beki wa kulia utaongezeka, huku Shomari Kapombe na David Kameta "Duchu" wakilazimika kupambana zaidi kuwania nafasi ya kuanza kikosini msimu wa 2026/27.
