Mamelodi yamtaka Lucas kurudi klabuni
Klabu ya Mamelodi Sundowns imempa taarifa kiungo mshambuliaji Lucas Ribeiro (27) kuwa arudi klabuni hapo ili kuwatumikia kuelekea msimu ujao wa 2026-27.
Lucas Ribeiro mpaka sasa yupo nyumbani kwao nchini Brazil baada ya kuachana na Curtural Leonesa ya Spain na ashafanya makubaliano ya awali na Al Ittihad SC ya Libya ili kujiunga nao kwa msimu mpya kwa ushawishi wa kocha Rhulani Mokwena.
Lucas Ribeiro anasubiri maamuzi ya FIFA ili afanye maamuzi ya mwisho kama atarudi Mamelodi Sundowns au atasaini mkataba wa Al Ittihad SC baada ya Sundowns kushitaki kuwa Lucas Ribeiro alivunja mkataba kimakosa bila kufuata taratibu zote hadi kujiunga na Curtural Leonesa.
