Lupini Mawuku ajiunga Azam FC

KLABU ya Azam FC imemtambulisha beki wa kati, Lupini Mawuku Dieumerci (20) kutoka AS Maniema Union ya kwao, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC).

Anakuwa mchezaji mpya wa tatu pamoja na beki mwingine, Henri Braham Stanic Mbelgiji mwenye asili ya DRC kutoka Stellenbosch FC ya Afrika Kusini.

Mwingine ni winga Muivory Coast, Kipré Tiagori Emmanuel Junior Zunon ‘Kipre Junior’ aliyejiunga tena na Azam FC akitokea MC Algiers ya Algeria.

Kipre Junior amerejea Azam FC ambako awali alicheza kuanzia msimu wa 2022-2023 akitokea SOL FC d’Abobo ya kwao, Ivory Coast hadi 2024-2025 alipohamia MC Algiers.


Machapisho maarufu kutoka blogu hii

FIFA yatoa orodha ya vilabu bora duniani, Simba na Yanga zachuana vikali

Beno Ngassa mdogo wa Mrisho Ngassa anayekipiga Tanzania Prisons

HISTORIA YA TIMU YA MASHUJAA YA KIGOMA, KUMBE NI SHEA YA JESHI NA WANANCHI