Kitambala kuondoka Azam kisa mshahara

Klabu ya Azam imeshindwa kulipa dola 150k ili kuendelea kumtumia mshambuliaji wao Japhet Kitambala ambaye alijiunga na Azam fc kwa mkopo akitokea Maniema.

Klabu ya Maniema imeiambia uongozi wa Azam ili mshambuliaji huyo aendelee kusalia Chamazi wanatakiwa kulipa dola 150k kitu ambacho Azam wamekataa.

Hivyo kufanya dili hilo kushindikana, lakini Singida Black Stars wamejaribu kuwasiliana na kambi ya Kitambala kuona namna ya kumpata mshambuliaji huyo lakini bado kambi ya mchezaji na klabu ya Maniema haijatoa majibu yenye muelekeo.

Ikumbukwe kuwa Kitambala haukuwa usajili wa moja kwa moja ulikuwa ni wa mkopo ili kama klabu itaridhika na huduma ya mshambuliaji huyo wafanye biashara ya moja kwa moja.

Lakini mpaka sasa matajiri wa Azam hawajaridhishwa na huduma ya mchezaji huyo ambae alijiunga na Azam dirisha kubwa la msimu uliopita.


Machapisho maarufu kutoka blogu hii

FIFA yatoa orodha ya vilabu bora duniani, Simba na Yanga zachuana vikali

Beno Ngassa mdogo wa Mrisho Ngassa anayekipiga Tanzania Prisons

HISTORIA YA TIMU YA MASHUJAA YA KIGOMA, KUMBE NI SHEA YA JESHI NA WANANCHI