Job kulipua bomu

Beki wa kati na nahodha msaidizi wa Young Africans SC, Dickson Job, ameibua mjadala mkubwa baada ya kuchapisha ujumbe kwenye ukurasa wake rasmi wa Instagram (@jobdick05) akidokeza kuwa atazungumza hadharani kuhusu jambo alilolieleza kuwa ni muhimu.

Kuna mtu nna ujumbe wake, Job aliandika:"Kama Nahodha, jukumu langu ni timu. Nidhamu ni bora kuliko kipaji. Hivyo nitazungumza kesho (Jumatatu). Sio busara mchezaji kurubuniwa."

Kauli hiyo imeibua hisia na maswali mengi miongoni mwa mashabiki wa Yanga na wadau wa soka, huku wengi wakisubiri kwa hamu kufahamu kile ambacho nahodha huyo msaidizi amesema atakiweka hadharani.

Ujumbe huo tayari umeanza kusambaa kwa kasi kwenye mitandao ya kijamii, ukiibua mijadala kuhusu kile kinachoweza kuwa kiini cha kauli yake.


Machapisho maarufu kutoka blogu hii

FIFA yatoa orodha ya vilabu bora duniani, Simba na Yanga zachuana vikali

Beno Ngassa mdogo wa Mrisho Ngassa anayekipiga Tanzania Prisons

HISTORIA YA TIMU YA MASHUJAA YA KIGOMA, KUMBE NI SHEA YA JESHI NA WANANCHI