Anicet Oura hatihati kubaki Simba
Kiungo mshambuliaji wa Simba SC, Anicet Oura, ameingia kwenye rada za klabu tatu za Ulaya kufuatia kiwango bora alichoonyesha tangu ajiunge na Wekundu wa Msimbazi mwezi Januari mwaka huu.
Taarifa zinaeleza kuwa Bursaspor (Uturuki), Víkingur Reykjavík (Iceland) na DAC 1904 Dunajská Streda (Slovakia) zinafuatilia kwa karibu hali ya nyota huyo wa Ivory Coast.
Bursaspor inaongoza mbio za kumsajili Oura na inatajwa kuwa tayari kuwasilisha ofa ya Euro 250,000. Hata hivyo, Kocha Steve Barker amesisitiza kuwa anahitaji kubaki na kiungo huyo kwa ajili ya msimu ujao.
Kwa tafsiri ndogo ni ngumu Simba Sc kumuuza Anicet Oura.
