Al Ittihad Iko tayari kumuuza Aziz Ki
Klabu ya Al Ittihad SC ya Libya ipo tayari kumuuza kiungo wao mshambuliaji Stephane Aziz Ki ikiwa ofa itafika mezani kwao itakayowaridhisha kuelekea msimu ujao wa 2026-27.
Al Ittihad SC imeshamlipa ada ya usajili na mishahara yote kwa Aziz Ki na imekanusha taarifa zilizovuma kuwa hawajalipa pesa hizo baada ya Young Africans SC umuhitaji kiungo Aziz Ki arudi klabuni kwao, Al Ittihad SC wanaheshimu mkataba wao na Aziz Ki na washalipa kila mchezaji ada yake ya usajili na mishahara.
