Machapisho

Inaonyesha machapisho kuanzia Aprili, 2026

Diamond amuibua tena P Diddy

Picha
Nyota wa muziki wa kizazi kipya Afrika mashariki na aliyejipatia umaarufu mkubwa barani Afrika na dunia kwa ujumla, Nasseb Abdul "Diamond Platinums" ameamua kuwajibu Watanzania waliokuwa wanavumisha kwamba yeye amewahi kufanya ufuksa na msanii mkubwa Marekani na duniani kwa ujumla P Diddy. 'Nikweli nilienda kwa P diddy Tulikaa Studio na Tulikaa Hadi usiku na Tulienda hadi kwenye Swimming Pool, Tulimkuta Diddy akiwa na wasanii wake wa 2 wakike na wakiume, Ila kuhusu hayo mambo mengine nivile tu hii nchi watu wanapenda kuhusisha watu na vitu vyakipuuzi tu. Yaani mimi nifanyiwe ujinga Tambwe yaani Mimi Lama simba Dangote kweli?" Alisema Diamond kupitia Wasafi Fm.

Keyekeh ahusishwa na Yanga msimu ujao

Picha
Kiungo wa ushambuliaji raia wa Tanzania Emmanuel Keyekeh mbioni kujiunga Young Africans, Keyekeh kiusili ni mzaliwa wa nchini Ghana ambaye kwasasa amechukua uraia wa Tanzania, Taarifa kutoka kwenye chanzo chetu zimetujuza kuwa Emmanuel Keyekeh (28) anaelekea kujiunga na Mtanzania Mwenzake Mohamed Damaro baada ya kutamatika msimu huu 2025/26, Mazungumzo baina ya Young Africans na viongozi wa juu wa klab ya Singida Black Stars yamefikia pazuri

Diamond Platinums afunguka makubwa kuhusu Mkubwa Fella

Picha
Hatimaye Diamond Platinums ameamua kufunguka ya moyoni ya kumuhusu meneja wake Said Fella "Mkubwa Fella" ambaye kwa sasa ni mgonjwa ambapo msanii huyo na CEO wa Wasafi amefunguka mengi. "Baada ya kuambiwa Mkubwa Fella nilijitolea kwakila kitu kuanzia Hospital hapa ndani na baadae nikampeleka hadi India kwa Gharama zote nilikuwa nalipa mimi, nilipokea mchango wa mtu aliejitolea Dola Elfu10 za kimarekani, Pesa hizo nilizichukua zote nikampa mkewe nikamwambia hii pesa wewe chukua utumie kwa matumizi ya nyumbani haya mengine ya Hospitali niachie mimi. Lakini nilikuja kuumia sana pale niliposikia Mke wa Mkubwa Fella anasema Mimi ninavyojitolea nakuwa kimbelembele kwenye maradhi ya mkubwa Fella nasababisha watu wengine wasimsaidie Mkubwa Baada ya hapo nikaamua kukaa pembeni" Amesema -Diamond Platnumz

Gomes afurushwa Saudi Arabia

Picha
Klabu ya Al Ahadalah inayoshiriki daraja la kwanza nchini Saudi Arabia imemfuta kazi aliyekuwa Kocha wake, Didier Gomes da Rosa kutokana na timu kufanya vibaya. Gomes amewahi kufundisha Simba SC kwa mafanikio makubwa.