Niffer akamatwa kwa kuhamasisha maandamano ya Oktoba 29

Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam limesema kwamba Leo, Tarehe 27,10,2025 majira ya saa 9 mchana eneo la Sinza Kumekucha limemkamata na linamuhoji Mwanamitandao na Mjasiriamali maarufu Jenifer Bilikwiza Jovin (Niffer) mwenye umri wa miaka 26 mkazi Masaki Peninsula Kinondoni kwa tuhuma za kuhamasisha vurugu na kuharibu miundombinu katika maeneo mbalimbali jijini hasa siku za kuelekea Uchaguzi Mkuu 2025.

Pia taarifa ya Jeshi imesema kwamba hatua zaidi za kisheria zinaendelea kuzingatiwa dhidi ya mtuhumiwa.

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

FIFA yatoa orodha ya vilabu bora duniani, Simba na Yanga zachuana vikali

Beno Ngassa mdogo wa Mrisho Ngassa anayekipiga Tanzania Prisons

HISTORIA YA TIMU YA MASHUJAA YA KIGOMA, KUMBE NI SHEA YA JESHI NA WANANCHI