Machapisho

Inaonyesha machapisho kuanzia Aprili, 2017

Simba warejea kileleni kwa kuiduwaza Mbao CCM Kirumba

Picha
Na Paskal Beatus. Mwanza Wekundu wa Msimbazi, Simba SC jioni ya leo imefanikiwa kukomboa mabao mawili na kufunga bao la ushindi ikiiadhibu Mbao FC mabao 3-2 mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara katika uwanja wa CCM Kirumba mjini Mwanza. Mbao FC walitakata kipindi cha kwanza na kufanikiwa kupachika bao la uongozi lililofungwa na George Sangija dakika ya 21 hali ambayo ilionekana kuwashitua Simba ambapo walilazimika kufanya mabadiliko ya haraka. Kikosi hicho cha Mbao ambacho kilionekana kuizidi Simba kiliongeza bao la pili kupitia kwa Evarigestus Bernard dakika ya 36 akipokea pasi ya Sangija muuaji wa bao la kwanza. Timu hizo zilienda kupumzika Simba ikiwa imelala kwa mabao hayo mawili, kipindi cha pili mpira uliendelea kuwa mgumu kwa Simba lakini walibadilika ghafla na kuweza kukomboa moja baada ya jingine yakifungwa na Muivory Coast, Fredrick Blagnon dakika ya 82 na 91. Mzamiru Yassin akapiga bao la tatu na la ushindi ambalo likaipeleka kileleni Simba ikifikisha pointi 58 n...

Yanga noma, yaitandika MC Alger 1-0

Picha
Na Ikram Khamees. Dar es Salaam Klabu bingwa ya soka Tanzania Bara, Yanga SC, jioni ya leo imechomoza na ushindi wa bao 1-0 katika Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam mchezo wa mkondo wa kwanza kombe la Shirikisho barani Afrika. Yanga imecheza soka zuri muda wote kuanzia kipindi cha kwanza na cha pili usipokuwa hawakuwa na bahati ya kupata mabao mengi na hiyo itawagharimu katika mchezo wa marudiano utakaofanyika Jumamosi ijayo huko Algeria. Hadi mapumziko timu zote mbili hazikufungana, kipindi cha pili Yanga waliendeleza mashambulizi langoni mwa wapinzani wao na dakika ya 60 waliweza kuandika bao la ushindi lililofungwa na Mzimbabwe Thabani Kamusoko. Kwa ushindi huo wa leo Yanga sasa inahitaji sare ya aina yoyote katika mchezo wa marudiano, na kama ikifungwa magoli mawili kwa bila itakuwa imetolewa mashindanoni

Kagera Sugar yaizuia Simba kukaa kileleni

Picha
Na Paskal Beatus. Bukoba Timu ya Kagera Sugar ya Bukoba mkoani Kagera, jioni ya leo imeizuia kabisa Simba SC ya Dar es Salaam kurejea kileleni mwa msimamo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara baada ya kuilaza mabao 2-1 katika Uwanja wa Kaitaba. Ikicheza mbele ya mashabiki wake, Kagera Sugar walicheza kandanda safi na kuwazidi maarifa Simba waliokuwa na sapota kubwa kutoka kwa mashabiki wake wa Kanda ya ziwa walioungana kuipa nguvu timu yao ili iweze kuzoa pointi tatu kila mchezo. Kagera Sugar inayonolewa na Mecky Mexime ilianza kupata bao kipindi cha kwanza lililofungwa na nyota wa zamani wa Simba, Mbaraka Yusuph Abeid ambaye pia ni mchezaji wa Taifa Stars. hadi mapumziko Kagera ilikuwa mbele kwa bao hilo, kipindi cha pili Kagera walirudi na kasi ile ile na kufanikiwa kuongeza bao la pili lililofungwa tena na mchezaji mwingine wa zamani wa Simba Edward Christopher "Eddo", Simba walipata goli la kufuta machozi lililofungwa na Muzamiru Yassin Kwa kipigo hicho sasa kinaifan...

Chirwa atimiza ahadi yake, aipeleka Yanga kileleni

Picha
Na Prince Hoza. Dar es Salaam Yanga SC leo imerejea tena katika usukani wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara baada ya kuilaza Azam FC bao 1-0 katika Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam. Hadi mapumziko miamba hiyo haijafungana hata bao, Azam walionekana kuutawala mchezo huo hasa kipindi cha kwanza lakini washambuliaji wake wakiongozwa na Yahaya Mohamed hawakuweza kufunga. Kipindi cha pili nacho kilikuwa cha Azam ingawa Yanga nao waliweza kuutawala kwa kiasi chake, Obrey Chirwa alipokea pasi maridadi ya kiungo Haruna Niyonzima ambapo hakuweza kufanya ajizi kwani alimchomoka beki wa Azam Daniel Amoah na kuipatia Yanga bao la ushindi dakika ya 70. Ushindi huo unaiweka Yanga kileleni ikifikisha pointi 56 ikiiacha Simba katika nafasi ya pili na pointi zao 55, Simba kesho wanacheza na Kagera Sugar katika Uwanja wa Kaitaba mjini Bukoba. Hata hivyo goli la Chirwa ni zawadi kwa mtoto wake mchanga ambaye aliahidi lazima afunge bao katika mchezo huo ili kupeleka zawadi kwa mwanaye huyo