Kagera Sugar yaizuia Simba kukaa kileleni

Na Paskal Beatus. Bukoba

Timu ya Kagera Sugar ya Bukoba mkoani Kagera, jioni ya leo imeizuia kabisa Simba SC ya Dar es Salaam kurejea kileleni mwa msimamo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara baada ya kuilaza mabao 2-1 katika Uwanja wa Kaitaba.

Ikicheza mbele ya mashabiki wake, Kagera Sugar walicheza kandanda safi na kuwazidi maarifa Simba waliokuwa na sapota kubwa kutoka kwa mashabiki wake wa Kanda ya ziwa walioungana kuipa nguvu timu yao ili iweze kuzoa pointi tatu kila mchezo.

Kagera Sugar inayonolewa na Mecky Mexime ilianza kupata bao kipindi cha kwanza lililofungwa na nyota wa zamani wa Simba, Mbaraka Yusuph Abeid ambaye pia ni mchezaji wa Taifa Stars.

hadi mapumziko Kagera ilikuwa mbele kwa bao hilo, kipindi cha pili Kagera walirudi na kasi ile ile na kufanikiwa kuongeza bao la pili lililofungwa tena na mchezaji mwingine wa zamani wa Simba Edward Christopher "Eddo", Simba walipata goli la kufuta machozi lililofungwa na Muzamiru Yassin

Kwa kipigo hicho sasa kinaifanya Simba ibaki katika nafasi ya pili na pointi zake 55 ikicheza mechi 25 wakati Yanga ambayo jana iliifunga Azam FC bao 1-0 inaongoza ligi hiyo ikiwa na pointi 56 mechi 25, Kagera sasa ni ya tatu ikiwa na pointi 46 ikiishusha Azam FC yenye pointi 44

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

HISTORIA YA TIMU YA MASHUJAA YA KIGOMA, KUMBE NI SHEA YA JESHI NA WANANCHI

STAA WETU: JEREMIA JUMA MTOTO WA JUMA MGUNDA ALIYEIKACHA SIMBA NA KUENDELEA NA UASKARI

MAKALA: SIMBA NI TIMU YA KWANZA TANZANIA KUINGIA NUSU FAINALI AFRIKA