Yanga noma, yaitandika MC Alger 1-0

Na Ikram Khamees. Dar es Salaam

Klabu bingwa ya soka Tanzania Bara, Yanga SC, jioni ya leo imechomoza na ushindi wa bao 1-0 katika Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam mchezo wa mkondo wa kwanza kombe la Shirikisho barani Afrika.

Yanga imecheza soka zuri muda wote kuanzia kipindi cha kwanza na cha pili usipokuwa hawakuwa na bahati ya kupata mabao mengi na hiyo itawagharimu katika mchezo wa marudiano utakaofanyika Jumamosi ijayo huko Algeria.

Hadi mapumziko timu zote mbili hazikufungana, kipindi cha pili Yanga waliendeleza mashambulizi langoni mwa wapinzani wao na dakika ya 60 waliweza kuandika bao la ushindi lililofungwa na Mzimbabwe Thabani Kamusoko.

Kwa ushindi huo wa leo Yanga sasa inahitaji sare ya aina yoyote katika mchezo wa marudiano, na kama ikifungwa magoli mawili kwa bila itakuwa imetolewa mashindanoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

HISTORIA YA TIMU YA MASHUJAA YA KIGOMA, KUMBE NI SHEA YA JESHI NA WANANCHI

STAA WETU: JEREMIA JUMA MTOTO WA JUMA MGUNDA ALIYEIKACHA SIMBA NA KUENDELEA NA UASKARI

MAKALA: SIMBA NI TIMU YA KWANZA TANZANIA KUINGIA NUSU FAINALI AFRIKA