Chirwa atimiza ahadi yake, aipeleka Yanga kileleni

Na Prince Hoza. Dar es Salaam

Yanga SC leo imerejea tena katika usukani wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara baada ya kuilaza Azam FC bao 1-0 katika Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.

Hadi mapumziko miamba hiyo haijafungana hata bao, Azam walionekana kuutawala mchezo huo hasa kipindi cha kwanza lakini washambuliaji wake wakiongozwa na Yahaya Mohamed hawakuweza kufunga.

Kipindi cha pili nacho kilikuwa cha Azam ingawa Yanga nao waliweza kuutawala kwa kiasi chake, Obrey Chirwa alipokea pasi maridadi ya kiungo Haruna Niyonzima ambapo hakuweza kufanya ajizi kwani alimchomoka beki wa Azam Daniel Amoah na kuipatia Yanga bao la ushindi dakika ya 70.

Ushindi huo unaiweka Yanga kileleni ikifikisha pointi 56 ikiiacha Simba katika nafasi ya pili na pointi zao 55, Simba kesho wanacheza na Kagera Sugar katika Uwanja wa Kaitaba mjini Bukoba.

Hata hivyo goli la Chirwa ni zawadi kwa mtoto wake mchanga ambaye aliahidi lazima afunge bao katika mchezo huo ili kupeleka zawadi kwa mwanaye huyo

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

HISTORIA YA TIMU YA MASHUJAA YA KIGOMA, KUMBE NI SHEA YA JESHI NA WANANCHI

STAA WETU: JEREMIA JUMA MTOTO WA JUMA MGUNDA ALIYEIKACHA SIMBA NA KUENDELEA NA UASKARI

MAKALA: SIMBA NI TIMU YA KWANZA TANZANIA KUINGIA NUSU FAINALI AFRIKA