Machapisho

Inaonyesha machapisho kuanzia Oktoba, 2016

Stewart Hall kuibukia KPL

Picha
Na Mrisho Hassan Kocha wa zamani wa mabingwa wa vilabu Afrika mashariki na kati, Azam FC, Stewart John Hall anatajwa kuwaniwa na mabingwa wa zamani wa Kenya, AFC Leopards inayoshiriki Ligi kuu ya Kenya (KPL). Leopards ambao jawafanyi vizuri kwa sasa, wanamtaka kocha huyo ambaye ana falsafa nzuri ya kucjeza soka la kushambulia na amewahi kuipa ubingwa wa vilabu Afrika mashariki na kati Azam FC. Tangu kuondoka kwa Hall ndani ya kikosi cha Azam, kimekuwa hakifanyi vizuri licha kwamba kinaongozwa na Wahispaniola wawili, Hall ataisaidia Leopards kurejea kwenye makali yake kama zamani

Dr Licky awatumbua Azam.TV, adai wachonganishi

Picha
Na Ikram Khamees, Dar es Salaam Mchambuzi wa soka nchini anayeheshimika kwa uchambuzi makini kwenye ngazi zote za kitaifa na kimataifa, akichambua bila upendeleo wala kupepesa macho, huku akijikita kwenye uhalisia zaidi, Licky Abdallah, maarufu kama Dr. Licky amewasulubu na kuwaponda warusha matangazo wa Azam TV kwamba wanakuza matukio kwa kuchezesha na kuchelewesha camera zao, na kuwachonganisha waamuzi wa mpira kwa Bodi ya Ligi. Amefafanua kwamba, ameangalia mechi zote za Simba SC na Young Africans weekend hii, na kugundua kwamba kila Yanga wanapofunga goli, wana-scroll camera zao ili ioneshe wameotea, hivyo kusababisha na kusambaza upotoshaji mkubwa kwa umma. Amesema ujanja huo amefafanuliwa na rafiki yake ambaye anaonesha matangazo ya Ligi Kuu ya Uingereza, kupitia TV1.

Kwa matokeo haya, Chelsea ni dhahili wanautaka ubingwa wa EPL

Picha
Na Nasri Alfan, Dar es Salaam Hii ni baada ya hapo jana kupiga Southampton Goli mbili kwa 0 Chelsea walipata magoli hayo kupitia kwa  Hazzard dk6 Costa dk55 Chelsea kwa sasa wame kua wakitumia mfumo wa 3-4-3 toka walipo pokea kipigo cha goli 3 kwa 0 kutoka kwa Aresenal kipindi hiko waki tumia 4-2-3-1 mfumo ambao uli wapa Chida wachezaji wa Chelsea Toka wa anze kutumia mfumo wa 3-4-3 Chelsea wame chinda michezo minne mfululizo uki wemo ule walio wapiga Manchester United goli 4 kwa 0 pale darajani Conte ame kua muumini wa mfumo huo toka akiwa Juventus pia Timu ya Taifa ya Ital na sasa Chelsea Mfumo ambao una onekana ume waingia kirahisi wachezaji wa Chelsea Huku waki watumia zaidi Golini 1. Thibaut Courtois Mabeki Azpilicueta  devid luiz Gery Cahil Viungo Victor mosses Nemanja Matic  Cante Marco Alonso Washambuliaji Pedro Rodrigues  diego costa Hazzard

Thomas Mashali auawa Dar

Picha
Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam Bondia wa ngumi za kulipwa nchini Thomas Mashali 'Simba asiyefugika' ameuawa usiku wa kuamkia leo na watu wasiojulikana huko maeneo ya Kimara jijini Dar es Salaam. Taarifa zilizopatikana ambazo zona uhakika zinasema Mashali alipigwa na watu waliokuwa na silaha za jadi ambao walidhani mwizi. Rafiki wa karibu wa bondia huyo aliyepata kutamba hapa nchini amesema marehemu hakuwa na tabia ya wizi, anasema huenda watu waliompiga walidhania mwizi ama baadhi ya watu wanaomfahamu walimwita mwizi ili apigwe hadi kufa. Rafiki huyo alizungumza huku akilia amedai Mashali ni mtu safi na wala hakuwa tabia ya ukorofi, lakini kuna taarifa nyingine inasema Mashali alikuwa kwenye ugomvi na wenzake hivyo aliwazidi nguvu na ndio maana wakamwitia mwizi na kupelekea kupigwa hadi kufa, maiti yake iliokotwa na waendesha bodaboda

Yanga yaichanachana Mbao

Picha
Na Salum Fikiri Jr, Dar es Salaam Mabingwa watetezi wa Ligi kuu Bara, Yanga SC, jioni ya leo katika uwanja wa Uhuru imeichanachana vibaya Mbao FC ya Mwanza kwa mabao 3-0 mchezo wa Ligi kuu ya Vodacom Tanzania Bara. Mbao ambayo ilichapwa bao 1-0 na Simba katika dakika za mwisho mpira kumalizika leo nayo ilikataa kuruhusu bao kipindi cha kwanza ambapo walienda mapumziko wakiwa suluhu, kipindi cha pili Yanga walikianza kwa kasi na kufanikiwa kupata bao la kwanza lililofungwa na Vincent Bossou ambaye ni beki wa kati. Yanga waliongeza bao la pili lililofungwa na mlinzi wa kulia ambaye pia hucheza nafasi zote za ulinzi Mbuyu Twite aliyeurusha mpira ulioingia wavuni ukiguswa na kipa wa Mbao  Amissi Tambwe aliongeza bao lake la saba na la tatu kwa Yanga. Kwa matokeo ya mcheo wa leo Yanga imefikisha pointi 27 huku ikiendelea kuifukuzia Simba inayoongoza Ligi ikiwa na pointi 32

Kwa Simba hii Inachapa tu

Picha
Na Prince Hoza, Shinyanga SIMBA SC jioni ya leo imeichapa Mwadui FC mabao 3-0 katika mchezo wa Ligi kuu Tanzania bara uwanja wa Kambarage mjini Shinyanga. Kwa ushindi wa leo Simba imefikisha pointi 32 na kuzidi kupaa kileleni mwa msimamo wa ligi, mabao muhimu ya Simba yalifungwa na washambuliaji wake Mohamed Ibrahim 'Mo' aliyefunga mawili na Ramadhan Shiza Kichuya. Simba imezidi kuiacha Yanga kwa tofauti ya pointi nane huku ikizidi kutimua vumbi

Pluijm arejeshwa kinguvu Yanga

Picha
Na Mrisho Hassan Baada ya kutangaza kujiuzuru kuinoa Klabu ya Yanga, Mholanzi Hans Van der Pluijm amerejeshwa kinguvu leo katika Klabu hiyo na Waziri wa mambo ya ndani Mhe Mwigulu Nchemba ambaye ni mpenzi mkubwa na shabiki namba moja wa timu hiyo. Taarifa za ndani zenye uhakika zinasema Pluijm ameombwa kurejea Yanga na mheshimiwa Mwigulu kwa vile ameiwezesha Yanga kufanya mambo makubwa katika kipindi chake alichoinoa timu hiyo, waziri huyo alizungumza na uongozi wa Yanga na kuwataka wamrejeshe haraka Mholanzi huyo kisha akazungumza na kocha huyo ili akubali kurejea Yanga. Tayari Mholanzi huyo ameombwa radhi na viongozi wa Yanga na huenda leo akaanza kusimamia mazoezi ya mwisho ya timu hiyo ambayo Jumapili itacheza na Mbao FC, mchezo wa Ligi kuu Bara, Pluijm ameipa Yanga mataji mawili ya Ligi kuu Bara, taji moja la kombe la FA na kuifikisha Yanga hatua ya makundi kombea Shirikisho barani Afrika

Habari/Picha: Hivi ndivyo Sibuka FM walivyokinukisha Tabata Mtambani Jumamosi

Picha
Picha/Habari na Prince Hoza Kituo cha utangazaji cha Sibuka Fm, Jumamosi ilikinukisha katika mitaa ya Tabata Mtambani ikiunguruma na kipindi chake kimoja cha michezo ya wiki kinachojulikana kama MBS kikiongozwa na mtayarishaji wake David Pasko. Kipindi hicho cha masaa mawili kilifana kwani watu wengi wakiwemo wadau wa michezo walijitokeza, pia wachezaji wa zamani nao walipata nafasi ya kuzungumzia machache kuhusu mchezo wa soka. Naye mtangazaji wa kipindi hicho David Pasko amesema huo ni utaratibu wa redio yao kuwafikia wasikilizaji wake kila mahari, amesema kila Jumamosi watatembelea maeneo mbalimbali kuhakikisha wanawafikia wadau wao pia kujua maendeleo ya soka nchini na sehemu husika Zedy Musa mchezaji wa zamani wa Bandari Mtwara (Kulia), katikati ni David Pasko na kushoto ni Nasri Khalfan. David Pasko (Kulia) akiwa na mwenzake Nasri Khalfan wakiandaa mambo kabla ya kuanza kipindi, kushoto kwao ni wadau walioudhuria Mambo yakiwa hayajaanza ilikuwa Tabata Mtambani hiyo ...

Chirwa mtamkoma wenyewe, aifungia mabao mawili Yanga ikiifunga Kagera Sugar 6-2

Picha
Na Saida Salum, Bukoba Mabingwa watetezi wa Ligi kuu ya Vodacom Tanzania Bara, Yanga Sc Jumamosi wamefufua matumaini baada ya kuichabanga bila huruma Kagera Sugar kwa mabao 6-2 Uwanja wa Kaitaba mchezo wa Kigi kuu Bara. Mshambuliaji aliyekuwa akibezwa sana na vyombo vya habari, Mzambia Obrey Chirwa alifunga mabao mawili peke yake wakati Mzimbabwe Donald Ngoma naye akifunga mawili. Magoli mengine ya Yanga yalifungwa na Deus Kaseke na Simon Msuva na kuifanya Yanga itoke na ushindi mnono huku ikifikisha pointi 21 ikiendelea kushikilia nafasi ya tatu wakiwa nyuma ya Stand United ambayo ililazimishwa sare 3-3 na Mtibwa Sugar. Mabao ya Kagera yalifungwa na Mbaraka Yusuphu, mechi nyingine kama ifuatavyo. Mtibwa Sugar 3 Stand United 3, African Lyon 2 Mbeya City 0, Majimaji 1 Ruvu Shooting 1, Ndanda 1 Mwadui Fc 2, Jumapili Simba itaikaribisha Toto Africans uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam

Manji awaita Wanayanga wote hata waliofukuzwa uanachama ili wamjadili

Picha
Kauli za Mwenyekiti YUSUPH MANJI leo kwenye Mkutano na waandishi wa habari. "Kwenye mkutano mkuu baada ya mimi kuzungumza upande wangu, nitatoka nje ili wanachama wapate uhuru wa kujadili na kutolea uamuzi" "Nawaomba wanachama wa Yanga wajitokeze kwa wingi kwenye mkutano mkuu Jumapili waweze kuchangia masuala ya msingi kwa maendeleo ya klabu yao ila kama hujalipa ada ya uanachama kwa miezi 6 mkutano hautokuhusu" "Ndani ya siku 90 baada ya kupewa ridhaa ya wanachama, tutaanza ujenzi wa uwanja wa mazoezi kwa timu"

Muzamiru azamisha jahazi la Mbao usiku

Picha
Na Prince Hoza, Dar es Salaam Jahazi la Mbao FC limezamishwa na kiungo Muzamiru Yassin katika dakika ya 86 na kuipa ushindi wa bao 1-0 Simba SC na kuendelea kujikita kileleni mwa msimamo wa Ligi kuu ya Tanzania bara, katika mchezo uliofanyika uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam. Mpambano huo ulikuwa mkali na wa kusisimua hasa kutokana na timu zote mbili kila moja ikitaka kuibuka na ushindi lakini bila mafanikio yoyote, hadi mapumziko hakuna timu iliyoona lango la mwenzake. Kipindi cha pili kilianza kwa kasi huku Simba wakionekana kulishambulia lango la Mbao lakini uimara wa mabeki wa Mbao uliwafanya Shiza Kichuya, Ibrahim Ajibu na Laudit Mavugo kushindwa kufunga. Kuingia kwa Fredrick Blagnon kulileta mabadiliko katika safu ya ushambuliaji ya Simba na kulitia msukosuko lango la Mbao na hatimaye kiungo Muzamiry Yassin kuandikisha goli la ushindi ambalo limeipa Simba pointi tatu muhimu na kufikisha pointi 26 ikizidi kukaa kileleni na kumuacha hasimu wake Yanga kwa tofauti ya pointi nane...

Muzamiru Yassin azamisha jahazi la Mbao

Picha
Na Prince Hoza, Dar es Salaam Kiungo Muzamiru Yassin amelizamisha jahazi la timu ya Mbao FC kutoka Mwanza katika mchezo wa Ligi kuu Bara uliofanyika uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam, wakati Simba SC iliposhinda bao 1-0 na kujiweka katika mazingira mazuri ya ubingwa. Vinara hao walijipatia bao hilo katika dakika za lala salama na kuamsha ndelemo kwa mashsbiki wake walioanza kukata tamaa kutokana na wapinzani wao Mbao kuonyesha kandanda safi huku mabeki.wake wakiwa makini kuwazuia washambuliaji wa Simba. Laudit Mavugo na Ibrahim Ajibu walishindwa kufurukuta mbele ya mabeki wa Mbao na kujikuta wanashindwa kufumania nyavu kama ilivyo kawaida yao, Shiza Kichuya naye alibanwa, Fredrick Blagnon ndiye aliyeingia na kubadili sura ya mchezo na Simba kupata bao la usiku. Kwa ushindi huo Simba imefikisha pointi 26 ikiwa imecheza mechi tisa na ikimuacha mtani wake Yanga kwa tofauti ya pointi 8

Waamuzi wapanga kugomea mechi zote za Coastal Union

Picha
Na Saida Salum, Dar es Salaam Imefahamika kwamba waamuzi wote wanaochezesha mechi za Ligi kuu Bara na Ligi Daraja la kwanza Tanzania bara, wamepanga kugomea kuchezesha mechi zote za Coastal Union ya Tanga kufuatia mashabiki wa timu kuwa na tabia ya kuwapiga na kuwajeruhi waamuzi. Hiyo imefahamika hasa kufuatia mashabiki wa Coastal kujitokeza uwanjani na kumpiga vibaya mwamuzi aliyekuwa akichezesha mechi yao na kumdhuru, Video iliyoenea mtandaoni ikimuonyesha mwamuzi aliyekuwa akichezesha mechi ya Coastal Union akipigwa na mashabiki wa Coastal. Licha ya mashabiki hao kutumia viti na chupa za maji kumpiga mwamuzi huyo aliyekuwa akiamuliwa na polisi mmoja ambaye naye alielemewa na kundi kubwa la mashabiki hao wahuni wa Coastal waliojifanya wana hasira kali, waamuzi wamesema hawatachezesha mechi za Coastal na wanashinikiza timu hiyo ifutwe

Je Simba itaweza kuitafuna Mbao?

Picha
Na Mrisho Hassan, Dar es Salaam Wekundu wa Msimbazi, Simba SC jioni ya leo inawakaribisha Mbao.FC ya Mwanza katika mchezo wa Ligi kuu Bara uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam. Mbao ambao katika siku za hivi karibuni imekuwa katika kiwango kizuri ikizitoa nishai timu ilizokutana nazo, hivyo hata katika mchezo wake na Simba leo unatajwa kuwa na ushindani. Simba ambayo ndiyo vinara wa ligi hiyo ikiwa na pointi 23 inatarajiwa kujiongezea pointi nyingine tatu ingawa si kirahisi mno kama inavyodhaniwa na mashabiki wake. Baada ya mchezo wa leo, Simba inajiandaa na mchezo mwingine dhidi ya Toto Africans ya Mwanza katika uwanja huo huo wa Uhuru, nyota Shiza Kichuya anatarajia kuonyesha tena cheche zake kama kwenye michezo iliyopita wakati timu hiyo ikitoa vipigo

Chirwa, Msuva waipaisha Yanga

Picha
Na Salum Fikiri Jr, Mwanza Viungo washambuliajj Obrey Chirwa raia wa Zambia na Saimon Happgody Msuva, jana jioni kila mmoja alifunga bao moja, Yanga SC ikiwazamisha wadogo zao Toto Africans 'Wana kishamapanda' mabao 2-0 uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza mchezo wa Ligi kuu Bara. Ushindi huo wa Yanga uliwafanya wafufue matumaini ya kuifukuzia Simba inayoongoza ligi hiyo, Yanga imefikisha pointi 18 ikiwa imeshuka dimbani mara 8, Chirwa alifikisha bao lake la pili tangu ajiunge na Yanga akitokea FC Platinum mwishoni mwa Julai. Goli hilo lilipatikana kipindi cha kwanza, kipindi cha pili Yanga wakaongeza bao la pili kwa mkwaju wa penalti iliyofungwa kistadi na Saimon Msuva, Matokeo mengine Prisons 2 Stand United 1, Mbeya City 1 Ndanda 1, Majimaji 2 African Lyon 0, Ruvu Shooting 1 Mwadui 1, na Azam FC 1 Mtibwa Sugar 1, leo Simba inacheza na Mbao ya Mwanza uwanja wa Uhuru

Yanga ya kimataifa yatikisa viwango vya ubora CAF

Picha
Na Salum Fikiri Jr, Dar es Salaam SHIRIKISHO la Soka Afrika (CAF) limetoa viwango vya ubora wa klabu barani, huku Yanga ikiongoza kwa klabu za Tanzania. Kwa mujibu wa taarifa ya Ofisa Habari wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Yanga SC imeshika nafasi ya 331 mbele ya Azam FC iliyo katika nafasi ya 351, wakati klabu nyingine ya Tanzania iliyoingia ni Simba SC iliyo katika nafasi ya 356.

Samatta atajwa kuwania tuzo ya mwanasoka bora Afrika

Picha
Na Mwandishj Wetu Mtanzania Mbwana Samatta ametajwa katika orodha ya majina 30 yatakayowania tuzo ya Mchezaji Bora Afrika kwa mwaka 2016 huku Yaya Toure akiachwa. Katika orodha hiyo wamo wachezaji wengine ambao ni Riyad Mahrez, Pierre-Emerick Aubameyang na Kelechi Iheanacho. Kutoka Afrika ya Mashariki pia wamo Victor Wanyama wa Kenya na Dennis Onyango wa Uganda.

Kumbe Said Ally aliyetobolewa macho na Scorpion ni shabiki wa kutupwa wa Simba

Picha
Na Prince Hoza, Dar es Salaam Kumbe yule jamaa aliyetobolewa macho na jambazi Scorpion, anayefahamika kwa jina la Said Ally Mrisho ni shabiki wa kutupwa wa Simba na ameweza kulia akiimbuka timu yake hiyo. Said Ally amemwaga machozi hasa akiililia Klabu yake hiyo kwani hatoiona tena machoni mwake, Said anaikumbuka Simba kwani alikuwa akienda kuitazama lakini ndio basi hawezi tena kuiona Simba yake. Anasema amewamisi wale mashabiki wakorofi waliong' oa viti uwanja wa Taifa Dar es Salaam, anakiri kama angekuwepo na yeye angeng' oa kwani ni mkerekwetwa haswa wa Simba, anawaomba mashabiki wenzake wa Simba wamuombee

Kichuya awa mchezaji bora Simba

Picha
Na Prince Hoza Winga na kinara wa mabao Ligi kuu ya Vodacom Tanzania bara, Shiza Ramadhan Kichuya, amechaguliwa kuwa mchezaji bora wa Klabu ya Simba wa mwezi Septemba mwaka huu. Kichuya ambaye ndiye kinara wa mabao Ligi kuu bara akiwa amefunga mabao sita, ameshinda tuzo ya uchezaji bora wa mwezi Septemba akiwa amefanya vizuri na kuiwezesha timu yake ya Simba kuongoza Ligi. Kufanya vizuri kwa nyota huyo kumenfanya awe mwanasoka bora, Kichuya aliyesajiliwa msimu huu akitokea Mtibwa Sugar ya Turiani Manungu wilayani Mvomelo mkoani Morogoro kwa sasa ndiye mchezaji anayeng' ara

Simba SC kuendeleza mauaji leo Uhuru

Picha
Na Salum Fikiri Jr, Dar es Salaam Vinara wa Ligi kuu bara, Simba SC, jioni ya leo inashuka uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam kuwakaribisha Wanamkurukumbi, Kagera Sugar kutoka Misenyi mkoani Kagera mchezo wa Ligi kuu bara. Mchezo huo utakuwa mkali kwakuwa kila timu inataka kushinda ili kujiweka katika mazingira mazuri, Simba ambao ndio wanaoongoza ligi hiyo wakiwa na pointi 20 wana uhakika mkubwa wa ushindi kutokana na wachezaji wake kucheza kwa kujituma. Shiza Kichuya ambaye ndiye kinara wa mabao kwa sasa akiwa amefunga mabao sita, anatarajia kuiongoza Simba leo katika mchezo huo wa tisa, Lakini mechi nyingine zitapigwa leo ambapo JKT Ruvu na Mwadui FC, Toto Africans na Majimaji, Mtibwa Sugar na Tanzania Prisons wakati Stand United itachuana na African Lyon

Mavugo apewa mechi sita Simba

Picha
Na Saida Salum Mshambuliaji wa kimataifa wa Simba SC  Laudit Mavugo raia wa Burundi, amepewa mechi sita na benchi la ufundi la timu hiyo na baada ya hapo atapigwa benchi kisha kutemwa msimu ujao. Mavugo alionyesha uwezo mkubwa kwenye mechi za mwanzo mwanzo na kuishia kufunga mabao matatu tu na kujikuta akishindwa kufurukuta kwenye mechi zilizofuata na kuwaudhi mashabiki wa timu hiyo. Tayari Wanasimba walishaanza kumpenda na kumtukuza kama Emmanuel Okwi, lakini ameanza kupoteza ukali wake na sasa si lolote, chanzo cha habari kinasema, Mavugo amewaudhi Simba baada ya kushindwa kuifunga Yanga na sasa uongozi wa Simba unahaha kumrejesha mshambuliaji wake wa zamani Mganda Emmanuel Okwi anayecheza soka la kulipwa Denmark

Adebayor amkingia kifua Bossou wa Yanga

Picha
Na Mwandishi Wetu Nahodha wa zamani wa Togo na mshambuliaji wa timu za Arsenal na Tottenham zote za England, Emmanuel Adebayor, ametamba kumkingia kifua beki na nahodha wa sasa wa timu ya taifa ya Togo, Vincent Bossou. Bossou ambaye pia ni beki tegemeo wa mabingwa wa soka Tanzania bara ameahidiwa kutafutiwa timu barani Ulaya na Mtogo mwenzake aliyewahi kutamba barani ulaya, Adebayor amesema atajitahidi kuhakikisha Bossou anapata timu msimu huu ama ujao. Naye beki huyo ametoa tamko kwamba yuko tayari kwenda Ulaya kama atapatiwa timu na Adebayot, lakini kama hajapata timu Ulaya basi ataendelea kuitumikia Yanga kwani ndiyo timu iliyomsukuma mpaka kufikia hapo halipo

Azam.FC hakukaliki hakulaliki, Bocco hatihati

Picha
Na Mrisho Hassan, Dar es Salaam Hali si shwari kwenye timu ya Azam FC ya jijini Dar es Salaam hasa kufuatia mwenendo mbaya wa timu hiyo katika Ligi kuu ya Tanzania bara inayoendelea ambapo hadi sasa imefikisha pointi 11 ikiwa imecheza mechi 8. Mabingwa wa Klabu Afrika mashariki na kati wameshapoteza mechi tatu, Jana Azam imelala bao 1-0 na Stand  United katika uwanja wa Kambarage mjini Shinyanga. Tayari Azam ilishafungwa na Ndanda FC mabao 2-1, Simba SC 1-0 na jana ikapoteza mchezo mwingine tena dhidi ya Stand, matokeo hayo yameifanya Azam ishikilie nafasi ya tisa ikiwa na pointi 11 ikicheza mechi nane. Hofu imemkumba nahodha wa timu hiyo John Bocco "Adebayor" yuko hoi akiwa na wasiwasi mkubwa kwani yeye alishatakiwa aondolewe kikosini na makocha wapya wa timu hiyo ambao ni raia wa Hispania, Bocco huenda akaachwa kutokana na ripoti ya kocha huyo itakapowasilishwa kwa uongozi kwakuwa hadi sasa hajafanya lolote

Yanga yaibanjua Mtibwa, Chirwa atoa gundu

Picha
Na Prince Hoza, Dar es Salaam Mabingwa watetezi wa Ligi kuu Tanzania bara, Yanga SC, jioni ya leo imeilaza Mtibwa Sugar ya Morogoro kwa jumla ya mabao 3-1 uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam. Yanga iliyotoka kwenye matokeo mabaya ya kulazimishwa sare ya 1-1 na watani zao Simba, walikuwa wa kwanza kupata bao lililofungwa na Mzambia, Obrey Chirwa ambaye leo ndio ametoa mkosi kwa kufunga bao lake la kwanza. Mtibwa Sugar ilisawazisha bao hilo katika kipindi cha pili kupitia kwa winga wake Haroun Chanongo, lakini wakazinduka na kuongeza bao la pili likifungwa na Simon Msuva kisha ikaongeza la tatu likifungwa na Donald Ngoma. Kwa matokeo hayo Yanga imefikisha pointi 14 ikiwa imecheza mechi saba, mechi nyingine kama ifuatavyo, Stand United 1 Azam FC 0, Mbao 3 Toto Africans 1

Simba yazidi kutakata kileleni

Picha
Na Saida Salum Vinara wa Ligi kuu Tanzania bara, Simba SC, jioni ya leo imeibuka na ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Mbeya City katika uwanja wa kumbukumbu ya Sokoine Mbeya. Ibrahim Ajibu alikuwa wa kwanza kuifungia bao Simba, kabla ya Shiza Ramadhan Kichuya kuongeza bao la pili, Hata hivyo Simba walikosa penalti iliyopigwa na Fredrick Blagnon. Kwa ushindi huo Simba inaendelea kujikita kileleni ikiwa na pointi 20 ikiwa imeshuka dimbani mara 8, Wekundu hao wa Msimbazi wanajiandaa na mchezo wao mwingine dhidi ya Prisons pia ya Mbeya. Nayo Mbao FC imeichapa Toto Africans mabao 3-1 katika uwanja wa CCM Kirumba

Simba na Yanga vitani tena leo

Picha
Na Saida Salum, Dar es Salaam Ligi kuu ya Vodacom Tanzania bara, inatimua vumbi tena leo kwa miamba ya soka nchini Simba na Yanga kujitupa katika viwanja tofauti kuwania pointi tatu muhimu. Miamba hiyo ina kumbukumbu ya kutoka sare ya 1-1 wao kwa wao juma lililopita katika uwanja wa Taifa, Dar es Salaam, Yanga leo watawaalika wakata miwa wa Mtibwa Sugar katika uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam. Wakati Wekundu wa Msimbazi, Simba SC watakuwa wenyeji wa Mbeya City katika uwanja wa Sokoine jijini Mbeya, Simba ndio vinara wa ligi hiyo wakiongoza na pointi zao 17 wakati Yanga wanashika nafasi ya sita na pointi zake 11

RNE YAMPONGEZA MENEJA WAO

Picha
Na Mwandishi Wetu, Tanga Uongozi wa R N E wampongeza meneja wao ndugu Juma Rashidi Shengoshi kwa kusimamisha harakati pia imewapongeza wasanii wake pamoja na mashabiki wake wote pia imefurahishwa na mashindano ya vipaji ya fanyika Tanga Korogwe Hale pia imewapongeza wadau wake wote ndani ya Tanga na njee ya Tanga kwa kuisimasha   rap newz entertiment

Pluijm atamba yeye ndiye kocha wa Yanga wengine wataishia magazetini tu

Picha
Na Mwandishi Wetu Kocha mkuu wa Yanga SC, Mholanzi Hans Van der Pluijm amesema yeye ndiye kocha mkuu wa Yanga na atambui kama kuna kocha mwingine atakuja kuinoa timu hiyo kwakuwa mpaka sasa hajapewa barua na mwajiri wake ya kuachishwa kazi. Akizungumza na mwandishi wa mtandao huu, Pluijm ameshangazqa na taarifa zilizosambaa kwenye kurasa mbalimbali za magazeti ya juzi na jana kwamba kuna kocha mpya anakuja kuchukua nafasi yake. Mholanzi huyo aliyeinoa Yanga kwa misimu miwili na kuipa taji mara mbili mfululizo la Ligi kuu bara, ameweka rekodi ya kufundisha Yanga kwa miezi 12 akicheza mechi 54 huku akipoteza mechi saba tu kitendo kinachodaiwa ni heshima kubwa mno kuwekwa, hivyo kocha mpya atakuwa na kazi kubwa ya kuivunja rekodi yake. Jana jina la Mzambia George Lwandamina ambaye ni kocha wa Zesco ametajwa kujiunga na Yanga akichukua nafasi ya Mholanzi huyo

Kumbe Julio katimuliwa Mwadui, Na sasa anasotea mgao wake

Picha
Na Ikram Khamees Siri zinazidi kuvuja, kumbe Kocha Jamhuri Kihwelu 'Julio' wa Mwadui hajajiuzuru kama alivyosema, nasemekana kocha huyo mwenye maneno mengi kuliko wote amefutwa kazi baada ya mwenendo mbaya wa timu yake. Taarifa ambazo Mambo Uwanjani ina uhakika nazo kwamba Julio amefutwa kazi na uongozi wa Mwadui ambao uko mbioni kupata kocha mpya na kilichobaki sasa ni kumpatia salio lake Julio. Mwenendo wa Mwadui kwenye Ligi kuu bara si mzuri na ulimpatia mecho kadhaa kocha huyo na kufikia tamati, Julio alitangaza hadharani kwamba ameamua kujiuzuru ukocha kutokana na marefa kumuhujumu

Goli la Tambwe limeondoka na mmoja

Picha
Na Ikram Khamees, Morogoro Kama ulikuwa haujui basi sikia hii. Goli lililofungwa dakika ya 26 kipindi cha kwanza na mshambuliaji hatari Amissi Tambwe raia wa Burundi na kuiandikia Yanga bao la kuongoza limesababisha kifo cha mshabiki wa Simba wa Dumila mkoani Morogoro. Shabiki huyo ambaye pia ni mwanachama, alipatwa na mauti baada ya kuanguka kwa presha wakati Tambwe akifunga bao hilo katika uwanja wa Taifa, Dar esSalaam. Mwandishi wa mtandao huu alizipata taarifa za shabiki huyo aliyeaga dunia ambaye alisafiri hadi Dar es Salaam kuhushuhudia mwenyewe mtanange huo,lilipoingia goli hilo, shabiki huyo alianguka kwa presha lakini baadaye akaanza kujisikia vizuri na kulazimika kurejea kwao Morogoro. Lakini kwa bahati mbaya akazidiwa ghafla na kufariki dunia huku chanzo kikidaiwa ni goli la Tambwe, Yanga na Simba zilitoka sare ya kufungana bao 1-1 uwanja wa Taifa, Dar es Sallaam

Kocha mpya Yanga huyu hapa

Picha
Na Shafih Hoza Yanga SC iliyokodishwa na kampuni ya Yanga yetu Limited, iko mbioni kumuajili kocha mkuu wa Zesco ya Zambia, George Lwandamina ambaye tayari ana rekodi mbili tofauti ambazo zimewavutia Yanga. Habari zilizotufikia hivi punde kuwa uongozi wa juu wa Yanga unataka kuachana na kocha wake wa sasa Mholanzi Hans Van der Pluijm hasa kwakuwa timu haifanyi vizuri ikiwa imeshika nafasi ya sita kwenye msimamo wa ligi kitendo kinachowaumiza vichwa Wanayanga. Lakini Hans Pluijm kama amewasikja viongozi wa Yanga kwani naye ameibuka na kusema anaanza ligi Alhamis ijayo Yanga itakapoikaribisha Mtibwa Sugar karika uwanja wa Uhuru Dar es Salaam. Lwandamina ameivusha Zesco hadi nusu fainali ya Ligi ya mabingwa barani Afrika, huku pia akiivusha timu ya taifa ya Zambia kwenye fainali za mataifa Afrika kwa wachezaji wa nyumbani maarufu CHAN, Mwenyekiti wa Yanga, Yusuph Manji anataka kuliondoa benchi lote la ufundi la Yanga na kumpa majukumu Mzambia huyo ambaye anakunwa na soka la Obrey Chir...

Mabondia kuzichapa Gongo la Mboto

Picha
Na Patrick Sambai Bondia mkongwe Mbaruk Heri anatazamiwa kuzichapa siku ya Jumamosi wakati michuano ya Goms Diwani Cup itakapofanyika katika uwanja wa Kampala uliopo Gongo la Mboto jijini Dar es Salaam. Akizungumza na Mambo Uwanjani, Mbaruk Heri ambaye aliwahi kuwa mwalimu wa bondia maarufu nchini Mada Maugo, amesema yuko tayari kuzichapa na bondia yoyote atayejitokeza siku hiyo. Michuano ya Goms Diwani Cup inafikia tamati siku ya Jumamosi kwa mechi ya fainali ya soka, pia kutakuwa na mashindano ya kuvuta kamba, kukimbia na gunia, kukimbiza kuku pamoja na ndondi. Hatua ya nusu fainali inafikiwa kesho kwa timu za Talent na Quality kuumana vikali wakati kesho kutwa Black Wizard na Mazombi, michuano hiyo inaratibiwa na diwani wa kata ya Gongo la Mboto Jakobo Kisi

Kifukwe ampasha Kiganja wa BMT

Picha
Na Mwandishi Wetu Mwenyekiti wa Baraza la wadhamini la Klabu ya Yanga, Francis Mponjoli Kifukwe amempasha katibu mkuu wa Baraza la Michezo la Taifa (BMT), Mohamed Kiganja kuwa uamuzi wa kuikodisha timu kwa Yusuf Manji umefuata taratibu zote na wala hawakukosea. Kifukwe amedai wao walifuata kila kitu kwa kufuata mwongozo kwa wanasheria wao wazoefu kama John Mkwawa na Alex Mgongolwa ambapo wakajiridhisha na kuamua kusaini mkataba wa kuikodisha Yanga kwa kampuni ya Yanga Yetu LTD iliyo chini ya Manji ambaye pia ni mwenyekiti wa Yanga SC. Kiganja alitakiwa kuuandikiwa barua uongozi wa Yanga ili kuomba ufafanuzi na si kuropoka kwenye vyombo vya habari kama alivyofanya, amedai wao hawazuiwi na baraza hilo ila baraza hilo linaweza kuwataka wabadili vipengele kama wameona hivyo

Kocha Mbeya City aigwaya Simba

Picha
Na Saida Fikiri, Mbeya Kocha mkuu wa Mbeya City, Mzambia Kinah Phiri ameonyesha kama anaigwaya Simba baada ya kusema kwa sasa ina kikosi kizuri lakini kamwe hatotishika na amepanga kujinyakulia pointi tatu. " Sina shaka sana na mechi ya Jumatano dhidi ya klabu ya simba kwani aina ya mpira wachezao Hauna tofauti sana na Huu wa kwetu ,  Nia yetu ni kuibuka na point 3 muhimu kwani nawajua vizuri simba na nina matumaini tele ya kuondoka na Ushindi " " Wachezaji wangu wamesema wapo tayari kwa mapambano na kila mmoja akisema lazima simba afungike hapa ,  Najua simba iko vizuri kwa sasa ila dakika 90 Zitaongea kwani Iliniuma sana kuambulia point 1 mbele ya stand United ikiwa tuliwakamata kila idara ila Nimeliona tatizo na nimelifanyia kazi " Hayo ni maneno ya kocha mkuu wa klabu ya mbeya City ,  Mzambia

Simba kuwafuata Mbeya City

Picha
Na Saida Salum, Dar es Salaam Vinara wa Ligi kuu ya Vodacom Tanzania bara, Simba SC, Jumamosi wanaanza safari ya kuelekea mkoani Mbeya ikiwa tayari kabisa kwa mecho zake mbili dhidi ya Mbeya City itakayocjezwa juma lijalo na mwingine dhidi ya Prisons. Kocha mkuu wa Simba, Mcameroon Joseph Marius Omog ameamua kuondoka na kikosi chake chote na ameahidi kupata pointi sita ingawa kocha msaidizi wa Mbeya City, Mohamed Kijuso ambaye aliwahi kuichezea Simba miaka iliyopita amedai Mbeya City ni kiboko ya Julio hivyo Simba waangalie wanaweza kukwama mbele yao

Mkwasa: Niko tayari kurudi Yanga

Picha
Na Prince Hoza Kocha mkuu wa timu ya taifa, Taifa Stars, Charles Boniface Mkwasa amesema yuko tayari kurejea Yanga endapo uongozi wa timu utafuata taratibu zote ikiwemo za kukubaliana na mwajili wake wa sasa TFF. Akizungumza hayo leo, Mkwasa amesema Yanga inaweza kumrejesha kwakuwa ndiyo iliyomfikisha hapo, 'Nitarejea Yanga kama watanihitaji, siwezi kukataa naiheshimu sana Yanga kwani nimekuja Stars nikitokea Yanga hivyo siwezi kushindwa kurejea watimize taratibu tu', alisema Mkwasa. Klabu ya Yanga inasemekana kwa sasa inataka kumrejesha kocha huyo hasa baada ya kuona haifanyi vizuri ikiwa chini ya Mholanzi Hans Van der Pluijm na msaidizi wake Juma Mwambusi kwani hadi sasa imeshacheza mechi sita za Ligi kuu bara ikiwa na pointi 11 wakati mpinzani wake Simba amecheza mechi saba lakini ana pointi 17 na anaongoza ligi huku Yanga ikiwa nafasi ya tatu nyuma ya Stand United yenye pointi 15. Tayari Yanga imeshapoteza mchezo mmoja na ikiwa imetoka sare mechi mbili huku ikikabiliwa ...

Mtangazaji wa BBC awa meneja Azam

Picha
Na Mwandishi Wetu Mtangazaji wa zamani wa idhaa ya kiswahili wa Shirika la Utangazaji la BBC, Abdul Mohamed ameteuliwa kuwa meneja wa timu ya Azam FC ya Dar es Salaam. Uteuzi huo ulioanza Oktoba 1, mwaka huu ni sehemu ya mikakati ya Azam Fc ya kujiendesha kiueledi na wakiamini ujio wa Mohamed atakayeingia kwenye sejretalieti ya timu, utaongeza nguvu kwenye eneo la uongozi na hatimaye kufikia malengo waliyokusudia. Azam FC inaamini katika uendeshaji mambo kiueledi ndani ya klabu  imekuwa na safu ya uongozi iliyosheheni watu wenye taaluma mbalimbali hivyo wanaamini kwa uzoefu aliokuwa nao Mohamed huko alikotoka akiwa kama Mwandishi wa habari kwenye shirika la utangaxaji (BBC) na nguvu kazi ya viongozi wengine utaweza kuifikisha Azam kwenye mafanikio

Simba waiomba radhi serikali

Picha
Na Prince Hoza Uongozi wa Klabu ya Simba, leo umetangaza kuiomba radhi serikalj ya Jamhuri ya muungano wa Tanzania chini ya rais John Pombe Magufuli kwa kitendo cha mashabiki wake kung' oa viti vya uwanja wa Taifa, Dar es Sakaam. Akizungumza na waandishi wa habari, Mkuu wa kitengo cha habari na mawasiliano wa Simba, Haji Sunday Manara, amesema leo kwamba Klabu ya Simba inaiomba radhi serikalj kufuatia vitendo vya kihuni vilivyofanywa na mashabiki wake. Manara amedai serikali imekuwa ikitumia fedha nyingi kuuendesha uwanja huo hivyo uharibifu uliofanywa na mashabiki wa Simba hautavumilika, aidha Manara ameiomba serikali kuwapa tena nafasi ya kuutumia uwanja huo. Wakati huo huo Klabu ya Simba leo imetangaza kamati mbalimbali ambazo zitahakikisha mnyama msimu huu ananyakua ubingwa wa bara baada ya misimu minne kuukosa, moja kati ya waliotangazwa kwenye kamati hizo ni Hassan Hasanoo, Juma Pinto na wengineo

Manji akabidhiwa Yanga rasmi

Picha
Na Paskal Beatus, Dar es Salaam BARAZA la wadhamini wla Klabu ya Yanga, limemkabidhi rasmi mfanyabiashara na mmiliki wa kampuni ya Yanga Yetu, Yusuf Manji timu kwa muda wa miaka kumi kama alivyoomba kwenye mkutano wa dharula uliofanyika Agosti 6 mwaka huu. Manji ambaye pia ni mwenyekiti wa klabu hiyo, amekabidhiwa timu leo mbele ya wadhamini wa klabu ambapo fomu ya makubaliano imesainiwa na kuanzia sasa Yanga ni mali ya Manji hivyo atakuwa akichukua asilimia 75 na wanachama wataambulia asilimia 25. Ndani ya mkataba huo suala la uwanja limechukua nafasi kubwa pamoja na timu kushika nafasi mbili za juu, hivyo wachezaji wazurina bora watakuwa wakisajiliwa kwenye kikosi hicho ambacho juma lililopita kililazimishwa sare na watani zao Simba ya kufungana bao 1-1. Yanga itakuwa imeandika historia ya kuwa klabu ya kwanza nchini kuendeshwa kikampuni kwani imefungua milango, Simba nao wako mbioni kumkabidhi timu mfanyabiashara kijana Mohamed Dewji

Hanspoppe aunga mkono mashabiki kung' oa viti Taifa

Picha
Na Mwandishi Wetu Mwenyekiti wa kamati ya usajili ya Simba SC, Zacharia Hanspoppe ameshangazwa na wale wote wanaokosoa kitendo cha mashabiki wa Simba kufanya vurugu kwa kung' oa viti. Hanspoppe akizungumza na chombo kimoja cha habarj (Siyo hiki) alisema ni bora kung' oa viti kuliko kung' oa meno ama vurugu nyingine ambazo zingelepelea madhara kwa mtu/watu. Kigogo huyo wa usajili amesema mwamuzi wa mchezo Martin Saanya ndiye aliyepaswa kubebeshwa lawama kwani yote yamesababishwa na yeye, "Mtu anauchukua mpira na mkono halafu anafunga goli, refa anakubali, huoni kama ni uvunjifu wa amani mbele ya maelfu ya watazamaji" alisema Hanspoppe

DEMBELE ASHANGAZA DUNIA

Picha
Karamoko Kadere Dembele mwenye umri wa miaka 13 jana ameweza kuishangaza dunia kwa kucheza mechi yake ya kwanza katika kikosi cha timu ya Celtic chini ya miaka 20. Dembele mwenye uwezo mkubwa wa kukaa na mpira ,kukimbia pamoja na nguvu aliingia katika dakika 81 katika mechi waliyoshinda 3-1 dhidi ya Hearts hapo jana. Mshambuliaji huyo ambaye wazazi wake ni wa Ivory Coast hana uhusiano wa kindugu na Moussa Dembele wa kikosi cha timu ya kwanza ya Celtic. ......... Wenzetu wana muendelezo Ulio bora zaidi , Ukitaka kuona Clips mbali mbali za huyu Kijana basi ni FOLLOW Instgram  Rjm Pilen  Alafu njooo Unambye Unampa asilimia ngapi 

SIKIA MANENO YA VICENT BOSSOU KUHUSIANA NA WASHAMBULIAJI WA LIGI KUU TANZANIA BARA .

Picha
Na Mwandishi Wetu BEKI wa kati wa mabingwa wa soka nchini Yanga SC, Vincent Bossou raia wa Togo ameibuka na kusema hakuna mshambuliaji anayemuumiza kichwa kwa sasa kwenye Ligi kuu bara, Bossou alicheza vizuri na kuwauzia washambuliaji wa kati wa Simba katika mchezo uliomalizika Jumamosi iliyopita uwanja wa Taifa Dar es Salaam. Mlinzi huyo ameiambia Mambo Uwanjani kuwa hajaona washambuliaji wenye uwezo wa kumpita, katika mchezo huo ulioisha kwa sare ya kufungana bao 1-1, Simba ilipata bao lake kwa mpira wa kona ulioingia moja kwa moja, hivyo washambuliaji wake watatu Ibrahim Ajibu, Laudit Mavugo na Fredric Blagnon walishindwa kupenya mbele ya beki huyo anayefahamika kama Kaka jambazi " Kwa sasa hapa Bongo sijaona mshambuliaji ambaye anaweza kunitisha wala kunifanya nimuwaze kukutana naye kwasababu wote nawaona wa kawaida na wengi wao wanaongea na tunapokutana nao wanakuwa na Viwango vya kawaida tofauti na wanavyoongea.

JAMALI MALINZI ASEMA HAYA KUHUSIANA NA SERENGETI BOYS .

Picha
Na Salum Fikiri Jr Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Jamal Malinzi amesema kwamba ataendelea kuwa karibu na vijana na Timu ya Tanzania ya vijana ‘Serengeti Boys’ licha ya kuondolewa na Congo kwenye harakati za kufuzu fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika kwa vijana zitakazofanyika Madagascar, hapo Aprili, mwakani.  Mipango ya TFF kwa sasa inayoongozwa na Malinzi kwa sasa ni kuiiingiza timu hiyo kwenye program ya timu ya vijana wenye umri wa chini ya miaka 20 maarufu kwa jina la Ngorongoro Heroes baada ya kuguswa na kilio cha vijana hao ambao walishindwa kujizuia kumwaga machozi mbele ya Malinzi ambaye alifanya kazi kubwa kuwatuliza pamoja na viongozi wengine. Serengeti Boys ilipoteza mchezo dhidi ya Congo Oktoba 2, 2016. Kwa kupoteza mchezo huo dakika ya pili kati ya nne ya nyongeza baada ya kumalizika kwa dakika 90, kumefanya vijana hao wa Tanzania kuenguliwa kwenye mashindano ya kuwania kucheza fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika – fainali zitakazofany...