Wachezaji Yanga wapewa likizo
Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam Yanga imewapa likizo fupi wachezaji wake hasa baada ya kuhairishwa kwa mchezo wao wa Ligi kuu bara dhidi ya JKT Ruvu uliokuwa uchezwe Jumatano ijayo. Wachezaji wa Yanga wameruhusiwa kurejea majumbani kwao huku wengine tisa wakijiunga kwenye timu za taifa zinazojiandaa na mechi zao za kufuzu fainali za mataifa Afrika mwishoni mwa wiki. Yanga Jumapili ikiyopita iliifunga African Lyon mabao 3-0 katika uwvja wa Taifa Dar es Salaam na kuanza ligi vizuri wakijikusanyia pointi tatu muhimu, shukrani kwa Deus Kaseke, Saimon Msuva na Juma Mahadhi waliokwamisha mipira nyavuni. Pia wachezaji wake wawili walipata pigo kwa kufiwa, kipa Deo Munishi 'Dida' alifiwa na baba yake mzazi aliyefariki katika hospitali ya Mwananyamala na kiungo Deus Kaseke akafiwa na babu yake