ENTENTE SETIF MABINGWA WAPYA BARANI AFRIKA

Klabu ya Entente Satif kutoka Algeria imeshinda ubingwa wa kilabu bora barani Afrika kwa mara ya kwanza katika miaka 26 baada ya kuishinda kilabu ya AS Vita Club kutoka jamhuri ya kidemokrasia ya Congo kutokana na mabao ya ugenini kufuatia sare ya 3-3 siku ya jumamosi.

Raundi ya pili ya fainali katika uwanja wa Mustapha Tchaker mjini Blida ilikamilika kwa sare ya 1-1,siku sita baada ya sare ya 2-2 katika mechi ya kwanza iliochezwa mjini Kinshasa.


Setif ilianza kuona lango na wapinzani wao dakika nne katika kipindi cha pili kupitia Sofaine Younes ambaye alifunga bao kupitia pasi ya El Hadi Belameiri.

Lakini wageni hao walisawazisha dakika tano baadaye kupitia Lema mabidi aliyepiga mkwaju kutoka nje ya eneo la kupigia penalti ili kuimarisha matumaini ya timu yake.

Mabidi pia alikuwa ameifungia kilabu hiyo mabao yake mawili katika raundi ya kwanza ya mchuano huo wikendi iliopita.

Bao hilo lilisababisha mechi hiyo kuwa ngumu ambapo Vita ilionyesha mchezo mzuri ikilinganishwa na wapinzani wao Setif waliojaribu kutumia mbinu chafu za kupoteza mda huku mashabiki wa kilabu hiyo wakitaka mchezo huo kukamilishwa kuanzia dakika ya 75.

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

HISTORIA YA TIMU YA MASHUJAA YA KIGOMA, KUMBE NI SHEA YA JESHI NA WANANCHI

STAA WETU: JEREMIA JUMA MTOTO WA JUMA MGUNDA ALIYEIKACHA SIMBA NA KUENDELEA NA UASKARI

MAKALA: SIMBA NI TIMU YA KWANZA TANZANIA KUINGIA NUSU FAINALI AFRIKA