BAYENR MUNICH WANA NJAA YA KUFUZU

Jerome Boateng 

Beki wa kushoto wa Bayern Munich, David Alaba amekariri kuwa magitu hao wa Ujerumani hawatapuuzilia kibarua chao dhidi ya klabu cha Italia, AS Roma kwenye ngoma ya Ligi ya Mabingwa wa Ulaya Jumatano licha ya kuwaadhibu kichapo kikali jijini Roma hivi majuzi. 

Bayern walilupua waitaliano hao 7-1 majuma mawili yaliopita kuhifadhi utawala wa kundi lao na alama zote tisa baada ya michuani mitatu huku wakiweka rekodi ya ushindi mkubwa sana ugenini ya mabingwa hao wa ligi ya Bundesliga ya Ujerumani katika shindano hilo la hadhi kuu.

Kiungo hatari wa Uholanzi, Arjen Robben, alifunga magoli mawili kuweka Bayern kwenye usukani wa Kundi E alama tano mbele ya Roma.

Vigogo hao watafuzi raundi ya 16-bora ikiwa watawakunguta tena wageni wao kwenye mechi ya marudiano itakayotandazwa ugani Allianz Arena kwa mara saba mtawalia.


“Roma ni timu kubwa na watakuja hapa kupigania alama zote. Wana wachezaji wenye uwezo wa kuamua mechi kibinafsi lakini bado tuna njaa na dhamira kuu ya kufuzu,” Alaba alibaini.

Kiungo wa Uhispania, Juan Bernat alionya mashabiki wao kutotarajia kichapo kingine cha mbwa watakapotoana kijasho na Roma.

“Itakuwa ni taswira tofauti kutoka ile ya mechi ya ugenini. Mkondo wa kwanza ulituendea vizuri sana na ilikuwa ni mechi ya kichaa lakini mambo sasa yataanza nguvu sawa,” Bernat alisema.

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

HISTORIA YA TIMU YA MASHUJAA YA KIGOMA, KUMBE NI SHEA YA JESHI NA WANANCHI

STAA WETU: JEREMIA JUMA MTOTO WA JUMA MGUNDA ALIYEIKACHA SIMBA NA KUENDELEA NA UASKARI

MAKALA: SIMBA NI TIMU YA KWANZA TANZANIA KUINGIA NUSU FAINALI AFRIKA