RONALDO KUIFIKIA REKODI YA RAUL LEO?

NYOTA wa Real Madrid, Cristiano Ronaldo anahitaji bao moja tu ili kulingana na mfungaji mabao anayeongoza kwenye Ligi ya Mabingwa Ulaya kwa miaka yote, Raul.

Real Madrid itakutana na Liverpool kwenye mchezo mkali wa Ligi ya Mabingwa hatua ya makundi leo Jumanne na Ronaldo ana nafasi kubwa ya kufikisha mabao 71 ambayo yalitundikwa na Raul au hata kupita zaidi atakapokuwa mbele ya mashabiki wa Santiago Bernabeu.

Madrid inaweza kufika katika hatua ya mtoano ya Ligi ya Mabingwa kama watawafunga Liverpool kwenye mchezo huo wa Kundi B

Ronaldo ambaye anatabiriwa kutwaa tuzo ya mchezaji bora wa dunia kwa mara nyingine hajapungua kasi. Amefunga katika mechi 12 mfululizo alizocheza katika siku za karibuni. Vile vile bao lake kwenye mechi dhidi ya Granada la Jumamosi ambapo walishinda mabao 4-0 lilimfanya kuwa mchezaji wa kwanza wa Real Madrid kufunga katika mechi nane mfululizo katika La Liga.


Msimu huu anaongoza katika jedwali la wafungaji kwenye Ligi ya Uhispania akiwa na mabao 17 na ana mabao 22 katika mechi zote msimu huu. Aliitungua Liverpool kwenye mchezo uliomalizika kwa ushindi wa mabao 3-0. Lakini Messi anamkimbiza akiwa na mabao 69.

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

HISTORIA YA TIMU YA MASHUJAA YA KIGOMA, KUMBE NI SHEA YA JESHI NA WANANCHI

STAA WETU: JEREMIA JUMA MTOTO WA JUMA MGUNDA ALIYEIKACHA SIMBA NA KUENDELEA NA UASKARI

MAKALA: SIMBA NI TIMU YA KWANZA TANZANIA KUINGIA NUSU FAINALI AFRIKA