Simba yafuata uchawi Zanzibar
Na Ikram Khamees. Dar es Salaam
Mabingwa watetezi wa Ligi Kuu Tanzania bara Simba SC wameelekea Zanzibar kwa ajili ya kuweka kambi kujiandaa na mchezo wa Ligi Kuu Bara dhidi ya mahasimu wao Yanga SC utakaopigwa Jumapili ijayo kwenye uwanja wa Taifa.
Simba itamkosa nahodha wake John Bocco "Adebayor" ambaye alionyeshwa kadi nyekundu katika mchezo wa Ligi Kuu bara dhidi ya Mwadui FC ambao Simba ilishinda mabao 3-1 uwanja wa Kambarage, inasemekana watani zao Yanga wameelekea mjini Morogoro