Yanga nao wafuata ndumba Moro
Na Mwandishi Wetu Homa ya mpambano we watani wa jadi katika soka la Tanzania imepamba moto ambapo tayari vilabu vikongwe vimeshaanza kulikimbia jiji la Dar es Salaam. Simba wao wameenda kujificha Zanzibar kwenye marashi ya karafuu wakati Yanga wameondoka zao kuelekea mji kasoro bahari Morogoro, Yanga na Simba zitaumana siku ya Jumapili kwenye uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam, katika mchezo uliopita Yanga iliifunga Singida United mabao 2-0