MKOLA MAN ASEMA DIAMOND NA JUX NI FREEMASON WALIOKOMAA
Na Mwandishi Wetu. Tanga
Mwanahip hop anayetamba na wimbo wake "Swali ndiyo jibu" , Christian Mhenga maarufu Mkola Man jana wakati akisherehekea siku yake ya kuzaliwa, 'Birthday' aliweka wazi majina ya wasanii wanaoamini Freemason hapa nchini.
Mkola Man ambaye naye alikuwa mmoja ya waumini wa imani hiyo inayodaiwa ni ya kishetani inayomfanya muumini wake kupata mafanikio ya haraka, aliwataja wasanii maarufu nchini wanaoshabikia imani hiyo.
Mambo Uwanjani ilikuwemo mjini Hale mkoani Tanga ambapo msanii huyo aliwaalika ndugu jamaa na marafiki zake ambapo aliweka wazi kuwa msanii Diamond Platinum ni nguzo ya freemason sambamba na Juma Jux na Young Killer.
Mkola Man ambaye alilazimika kuhama kwao kisa kutumikia imani hiyo kabla ajawaangukia wazazi wake na kutubu, amedai wasanii hao wamekuwa watumwa wa imani hiyo kwa kuvaa vidani vinavyoaminika kuwa vya freemason