MR CHEKA AJA KIVINGINE

Anselim Malembo ndio jina lake halisi lakini mashabiki wake wanamfahamu kwa jina la Mr Cheka hasa kutokana na wimbo wake uliopata kutamba katika miaka ya mwanzoni 2000 uitwao 'Mr Cheka' aliomshirikisha Mheshimiwa Temba, hatimaye msanii huyo ametangaza kurejea tena kwenye gemu.

Safari hii Mr Cheka ameamua kuwashirikisha wakongwe waliopata kutamba kitambo Juma Nature 'Kibra' na Mchizi Mox, akizungumza na Mambo uwanjani, Mr Cheka amesema tayari ameshatengeneza audio na wakongwe hao iitwayo 'Nacheka' ambapo amedai ni maombi ya mashabiki wake waliomtaka arudi katika muziki.


'Niliacha muziki nikiamini basi tena sitaweza kurejea, lakini kila ninapokwenda nakutana na mashabiki wanaonifahamu na wote wakinitaka nirejee, wengi wape sasa nimerudi nimeamua kuwafuata wakongwe Nature na Mchizi Mox na kufanya nao ngoma hii katika studio za Ozz zilizopo Tabata chini ya prodyuza Succh', alisema.

Wimbo huo ndio kama ujio wake mpya kwani tayari ameshaandaa nyimbo nyingine ambazo ataziachia hivi karibuni, pia nyota huyo wa muziki wa kizazi kipya amesema video ya wimbo huo iko njiani na muda wowote itakuwa tayari.

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

HISTORIA YA TIMU YA MASHUJAA YA KIGOMA, KUMBE NI SHEA YA JESHI NA WANANCHI

STAA WETU: JEREMIA JUMA MTOTO WA JUMA MGUNDA ALIYEIKACHA SIMBA NA KUENDELEA NA UASKARI

MAKALA: SIMBA NI TIMU YA KWANZA TANZANIA KUINGIA NUSU FAINALI AFRIKA