Machapisho

Bodi ya Ligi yainusuru Simba kwa Tabora United

Picha
Na Ikrwm Khamees Bodi ya Ligi (TPLB) imeiondoa mechi kati ya Simba na Tabora United iliyopangwa kuchezwa Disemba 28, 2024 sasa itapangiwa baadaye. Pia mchezo dhidi ya Simba na Singida Big Stars ambao awali haukupangiwa tarehe sasa utachezwa Disemba 28, 2024 kwenye Uwanja wa Liti mkoani Singida. Mchezo dhidi ya Tabora United ambao ulipangwa kuchezwa Disemba 28, 2024 kwenye Uwanja wa Ali Hassan Mwinyi mkoani Tabora umeondolewa na utapangiwa tarehe mpya. Kusogezwa kwa mechi ya Simba na Tabora United ambayo sasa ni moto wa kuotea mbali baada ya kuzifunga Yanga na Azam na kuigomea Singida Black Stars, Bodi ya Ligi ni kama wameisaidia Simba kutoka kwenye kichapo kwa walina Asali hao wa Tabora.

KMC yaikausha Pamba jiji

Picha
KMC ya Manispaa ya Kinondoni jijini Dar es Salaam wameikausha Pamba Jiji FC ya Mwanza bao 1-0 m hezo wa Ligi Kuu bara uwanja wa KMC Mwenge jijini. Bao pekee lililoipa pointi tatu muhimu limefungwa na Hance Masoud dakika ya 88, hata hivyo Pamba Jiji inayonolewa na Fred Minziro imecheza vizuri isipokuwa bahati haikuwa yao

Singida Black Stars yaipigisha kwata Prisons

Picha
Timu ya Singida Black Stars imeichapa Tanzania Prisons mabao 2-0 mchezo wa Ligi Kuu bara uwanja wa Kumbukumbu ya Sokoine mjini Mbeya. Mabao ya Singida Black Stars yamewekwa kimiani na Marouf Tchakei na Kennedy Juma, huo ni mwendelezo mzuri wa ushindi kwa Singida Black Stars inayonolewa na kocha wa muda Ramadhan Nswazurimo

Simba sasa ni ya tatu kombe la Shirikisho

Picha
Timu ya Bravo's de Maquis ya Angola kwasasa ndio wanaongoza kundi A kombe la Shirikisho barani Afrika huku Simba SC ya Tanzania ikishika nafasi ya tatu. Kwa mujibu wa msimamo wa kundi hilo uliopostiwa jana baada ya kumalizika kwa mechi zote, Bravo's wamekaa kileleni wakiiengua CS Constantine ya Algeria zote zikiwa na pointi 6. Lakini Simba SC ya Tanzania iliyokuwa inashika nafasi ya pili, sasa imeangukia nafasi ya tatu ingawa Ina pointi 6, CS Faxien ya Tunisia inashika mkia ikiwa haina hata pointi moja ingawa bado ina nafasi ya kwenda robo fainali.

Elie Mpanzu rasmi kuichezea Simba SC

Picha
Hatumaye kimaeeleweka kwa kiungo mshambuliaji Elie Mpanzu raia wa DR Congo kuidhinishwa katika kikosi cha Simba SC msimu huu. Mpanzu jana aliidhinishwa kwenye kikosi cha Simba na kuchukua nafasi ya kipa Ayoub Lakred, kwa maana hiyo Mpanzu ataitumikia Simba na kwenye mchezo wa keshokutwa dhidi ya KenGold huenda akavaa jezi kwa mara ya kwanza.

Prof Kabudi aishika pabaya Simba

Picha
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Prof. Palamagamba Kabudi akemea vikali uharibifu wa viti uliofanyika katika Uwanja wa Benjamin Mkapa katika mchezo wa Kombe la Shirikisho Barani Afrika kati ya Simba Sports Club ya Tanzania na CS Sfaxien ya Tunisia, Desemba 15, 2024. Prof. Kabudi amemuagiza katibu wa Wizara hiyo kuchukua hatua mara moja kwa kuwaandikia klabu ya Simba na kuwanakili Shirikisho la mpira nchini (TFF) kwa makusudi ya kuwataka walipie gharama za uharibifu zilizofanywa katika mchezo huo wa kombe la shirikisho Afrika. Pia Prof. Kabudi ameliagiza jeshi la polisi kuwasaka wote waliohusika kwenye uharibifu huo wachukuliwe hatua za kisheria.

Bravo's yashinda, kundi sasa lishakuwa gumu

Picha
Timu ya Bravo's de Maquiz ya Angola usiku huu imelitia shaka kundi lake lenye timu za Simba SC, CS Constantine na VS Faxien baada ya kuifunga CS Constantine ya Algeria mabao 3-2 mchezo wa kombe la Shirikisho kundi B. Ushindi huo unaifanya Bravo's kufikisha pointi 6 hivyo sasa timu zote tatu kulingana pointi, Simba ya Tanzania itakuwa na kazi ngumu kwani itasafiri kuzifuata Bravo's yenye pointi 6 na CS Faxien ambayo haina pointi. Ugumu wa kundi hilo unakuja kwa Bravo's kuitaka nafasi sawa na CS Constantine nayo kuitaka nafasi, huku Simba pekee ikisaliwa na mchezo mmoja nyumbani.