Kiungo wa Yanga, Moussa Balla Conte, ametumiwa salamu za nguvu na kocha wake wa zamani Alexander Dos Santos, akimtaka kupambana na kurejesha heshima yake ndani ya mabingwa hao.
Santos, aliyewahi kumfundisha Conte akiwa CS Sfaxien, amesema kiungo huyo ana kipaji kikubwa na haipaswi kukata tamaa kwa kutopata nafasi ya kucheza.
Anamtaka afanyie kazi maeneo ambayo wachezaji wenzake wanamzidi kisha aongeze mazoezi binafsi ili kurudi kwenye ubora wake.
Ameeleza kuwa Conte ni kiungo wa kisasa mwenye uwezo wa kupiga pasi ndefu, kukaba kwa nguvu na kuiongoza timu, akisisitiza kuwa tatizo linaweza kuwa kujiamini tu.
Santos: “Conte ni mchezaji mzuri, anaweza kurudi kwenye kiwango chake kama akijipanga na kuongeza kazi ya ziada.”
