Watoto wa wanamuziki, wageuka lulu mwenye soka

Dr Remmy Ongalla wa Ochestra Matimila na Bwammy Walomuna wa Ochestra Mangelepa
Viongozi wa bendi za Muziki huku watoto wao wakiwa miamba ya Soka.

Kali Ongala (jina kamili Kalimangonga Sam Daniel Ongallah Rampling) ni mwanasoka wa zamani na kocha wa mpira wa miguu kutoka Tanzania.

Ni mtoto wa mwanamuziki mashuhuri wa Tanzania, marehemu Remmy Ongala, alizaliwa tarehe 31 Agosti 1979 jijini London, Uingereza. Licha ya kuzaliwa Uingereza, alikulia na kupata malezi yake jijini Dar es Salaam, Tanzania, ambapo alianza kupata hamu ya michezo na soka tangu utotoni.

Safari yake ya soka ilianza rasmi mwaka 1999 alipojijiunga na Young Africans SC (Yanga) kutoka Bajaro FC, akijitengenezea sifa kama kiungo mshambuliaji mwenye ufundi mkubwa.

Baada ya mafanikio yake nchini Tanzania, alifanya majaribio ya kucheza soka nchini Uingereza na Marekani kabla ya kupata mikataba ya kucheza nchini Uswidi, akichezea klabu za FC Väsby United na GIF Sundsvall kati ya mwaka 2007 na 2011.

Baada ya kustaafu kutoka soka la kitaalamu, Kali Ongala aliendeleza taaluma yake katika ukocha.

Amehudumu kama kocha katika Azam FC, na hivi karibuni ameiungia KMC FC kama kocha mkuu, akiwa na dhamira ya kukuza soka la ushindani na kuendeleza vipaji vipya nchini Tanzania.

Christian Bwamy

Christian Bwamy ni mtoto wa mwanamuziki maarufu Bwanny Walomuna na kiongozi wa Ochestra Mangelepa, Christian ni mchezaji wa zamani wa soka wa Kenya aliyecheza kama mshambuliaji.

Alitumikia Gor Mahia, moja ya klabu mashuhuri zaidi nchini Kenya, na pia aliwahi kuwa sehemu ya timu ya taifa ya Kenya, Harambee Stars.

Safari yake
Christian Bwamy alisajiliwa na Gor Mahia mwaka 2007 akitokea Shule ya sekondari Jamhuri, alisifiwa kwa uwezo wake mkubwa wa kumiliki mpira, kasi, na akili uwanjani kama kiungo mshambuliaji.

Baada ya msimu mmoja tu na Gor Mahia, alihamia Norway mwaka 2008 kujiunga na klabu ya Follo FK kupitia ushirikiano wa MYSA, ambapo aliendeleza taaluma yake ya soka katika ligi ya Norway.

Alipata wito wa kwanza wa timu ya taifa ya Kenya, Harambee Stars, mwaka 2012 kwa ajili ya mechi dhidi ya Togo, ingawa hakucheza.

Baada ya kupata jeraha baya mwaka 2016 lililomzuia kucheza kwa kiwango cha juu, alitangaza kustaafu rasmi kutoka soka Januari 1, 2020. Baada ya kustaafu, Bwamy amegeukia taaluma ya sheria

Hapo alihitimu na kuwa wakili, na sasa anafanya kazi katika idara ya sheria ya serikali ya kaunti ya Oslo, Norway.

Kwa ufupi, Bwamy ni mfano wa mchezaji aliyehamia taaluma nyingine baada ya kustaafu soka, akiunganisha mafanikio ya michezo na taaluma ya kitaaluma.

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

FIFA yatoa orodha ya vilabu bora duniani, Simba na Yanga zachuana vikali

HISTORIA YA TIMU YA MASHUJAA YA KIGOMA, KUMBE NI SHEA YA JESHI NA WANANCHI

Beno Ngassa mdogo wa Mrisho Ngassa anayekipiga Tanzania Prisons