UKRISTO NI CHIMBUKO LA UYAHUDI
Inaandikwa na Fikiri Salum
UKRISTO (kutoka neno la Kigiriki, Khistos, ambalo linatafsiri lile la Kiebrania Masia, linalomaanisha "mpakwa mafuta" ni dini inayomwamini Mungu pekee kama alilivyofunuliwa kwa Waisrael katika historia ya wokovu ya Agano la kale la hasa Yesu Kristo katika Agano jipya ambaye ni mwanzilishi wake katika karne ya 1.
Dini hiyo iliyotokana na Ile ya Uyahudi, inalenga kuenea kwa binadamu wote, na Kwa sasa ni kubwa kuliko zote duniani ikiwa na wafuasi 2, 400, 000, 000 sawa na asilimia 33 kati ya watu 7, 274 bilioni ambao nusu ya pili wamegawanyika kati ya Waorthodoksi (asilimia 11, 9) na Waprotestant (asilimia 38,) wa madhehebu mengi sana.
Karibu wote wanakubali utatu mtakatifu yaani kwamba milele yote Mungu ni nafsi tatu zenye umoja kamili, baba, mwana na roho mtakatifu, ni kwa jina lao, kwamba mataifa yote wanahimizwa kubatizwa kwa maji Ili kuzaliwa upya, kadri ya agizo la Yesu ni kuingizwa katika fumbo la Mungu pekee kupitia fumbo la kifo na ufufuko wake mwenyewe.
Wakati wa mababu wa kanisa misingi ya imani ya Ukristo ilifafanuliwa na mitaguso ya kiekumeni namna inayokubaliwa na wengi kabisa kati ya Wakristo wa leo.
Maungamo yao yanakiri kwamba Yesu ni mwana wa Mungu aliyefanyika mtu Ili kuwaokoa binadamu, baada ya kuteswa na kuuawa msalabani alizikwa ila akafufuliwa siku ya tatu akapaa kwa Mungu akishiriki mamlaka ya baba hadi atakaporudi kuhukumu waadilifu na wasioabudu, akiwapa tuzo au adhabu ya milele kadiri ya imani na matendo yao.
Hivyo katika ya madhehebu ya Ukristo karibu yote yanamkiri Yesu kuwa kwa pamoja Mungu kweli na mtu kweli kwa umoja na nafsi yake ya Kimungu zinapatikana sasa hali hizo zote mbili.
Yote yanamkiri kuwa mkombozi wa watu wote, na kuwa ndiye atakayerudi mwishoni mwa dunia kwa hukumu ya wote, ingawa maelezo kuhusu jambo hilo yanatofautiana.
Vilevile yote yanamchukua kama kielelezo cha utakatifu ambacho kwa msaada wa roho mtakatifu na sakramenti zilizowekwa na Yesu mwenyewe, kuanzia Ile la ubatizo - kiwaongoze ndani ya kanisa katika maadili yao maalum kuanzia unyenyekevu na upole hadi upendo unaowaenea wote, bila kumbagua yeyote hata adui.
ASILI
Chimbuko la Ukristo ni mtu huyo aliyezaliwa takribani miaka 2000 iliyopita huko mashariki ya kati katika kijiji cha Bethlehemu kilichopo hadi hivi leo kwenye mipaka ya Palestina, alikuwa akiitwa Yesu wa Nazaleti (kijiji alikokulia) au mwana wa Yosefu mchonga samani, mama yake akifahamika kwa jina la Bikira Maria.
Kwa kumwita pia Kristo, wafuasi wake walikiri kwamba ndiye aliyetimiza utabiri wa manabii wa kale, kama unavyopatikana katika vitabu vya biblia ya Kiebrania na Deuterokanoni.
Habari za maisha na mafundisho yake zinapatikana kirefu zaidi katika Injili nne zilizokubalika, katika Agano jipya kwa jumla, lakini pia ziliandaliwa na kutabiriwa na Agano la kale.
YESU KAMA MASIA ALIYETABIRIWA
Ukristo ni matokeo ya utume wa Yesu, uliopokewa na waliomwamini kuwa ndiye Masia, yaani mkombozi aliyetimiliza ahadi za Mungu kwa binadamu.
Katika kitabu cha Mwanzo tunasoma utabiri wa kuja kwake ulianzia katika bustani ya Edeni pale Mungu alipomwambia nyoka, yaani shetani kuhusu mwanamke kwamba "uzao wake utakuponda kichwa", (Mwa 3: 15).
Baadaye Abrahamu, babu wa taifa la Israel kwa imani na utiifu wake Kwa Mungu, aliahidiwa kwamba katika uzao wake mataifa yote yatabarikiwa.
Musa mwanaharakati aliyewakomboa watu wa Israel kutoka utumwani Misri takribani miaka 1250 KK (Kabla ya kuzaliwa kwa Yesu), ndiye nabii wa kwanza kutabiri wazi kwa niaba ya Mungu ujio wa Masia au Kristo (Kumb 15: 15- 22, hususani mstari wa 18).
INAENDELEA
