UKRISTO NI CHIMBUKO LA UYAHUDI- 7

Inaandikwa na Fikiri Salum

Ilipoishia 

BAADAYE akawa katika mji mkubwa wa Antiokia, katika taarifa ya Luka tumemwona tena Yerusalemu alipokutana na Paulo na kushauriana juu ya kupokea wapagani katika Ukristo.

Endelea

Agano jipya ina nyaraka mbili zilizoandaliwa kwa jina lake, kumbukumbu ya kale inasema alifika mpaka Roma, hapo aliuawa pamoja na Paulo katika mateso ya kwanza ya Wakristo chini ya serikali.

Petro ni mfano mzuri wa nguvu na udhaifu katika maisha ya Kikristo, alikuwa na moyo mkuu kumtetea Yesu kwa upanga asikamatwe- lakini mpaka siku Ile hakuelewa kwamba njia ya Yesu si njia ya silaha.

Alitaka kuwa karibu na Yesu lakini kwa hofu akamkana, alimwingiza katika kanisa jemedari mpagani lakini baadaye akawaogopa waliosema kwamba mpagani asiingie katika ushirika mpaka awe ametahiriwa na kuwa Myahudi kwanza.

Mwishoni mwa maisha yake, Petro akawa shahidi wa damu kwa bwana wake kule Roma akafa msalabani kama Yesu.

Kanisa la Roma linamkumbuka kama Askofu' wake wa kwanza, kila Papa wa kanisa katoliki "huitwa mwandamizi wa Petro" kwani anashika cheo cha Askofu' wa Roma kinachoaminika kuwa cha kwanza kati ya Maaskofu wote duniani.

PAULO

Paulo hakuwa mfuasi wa Yesu alipokuwa duniani, alikuwa Mhayudi farisayo mzaliwa wa Tarso (mji wa Kilikia, leo nchini Uturuki) alikwenda Palestina kwa masomo ya kidini, tunasikia habari zake alivyohusika na kifodini cha Stefano (Mdo 6).

Aliposafiri hadi Dameski (mji mkuu wa Syria) kwa ajili hiyo, Yesu alimtokea katika ono akaongoka, kuwa Mkristo hivyo mtesaji wa Wakristo akawa mhubiri mkuu wa Injili.

Hakuna mwingine kati ya mitume wote aliyesafiri, kuhubiri na kuanzisha shirika kama Paulo, katika safari kubwa tatu alizunguka Asia magharibi na Ulaya kusini, akaendelea kufundisha shirika alipoondoka kwa njia ya barua (au nyaraka).

Nyaraka zake mbalimbali zimehifadhiwa katika Agano jipya, katika nyaraka hizo, Paulo anaonekana kuwa mtaalamu wa sheria za Kiyahudi ilivyo katika Agano la kale.

Akatetea kupokea wapagani katika kanisa akafundisha jinsi gani uhuru katika Kristo unavyopita masharti ya sheria ya kale.

INAENDELEA 


Machapisho maarufu kutoka blogu hii

FIFA yatoa orodha ya vilabu bora duniani, Simba na Yanga zachuana vikali

HISTORIA YA TIMU YA MASHUJAA YA KIGOMA, KUMBE NI SHEA YA JESHI NA WANANCHI

Beno Ngassa mdogo wa Mrisho Ngassa anayekipiga Tanzania Prisons