UKRISTO NI CHIMBUKO LA UYAHUDI - 12
Inaandikwa na Fikiri Salum
Ilipoishia
KWA kweli karne za kati zilikuwa na mchanganyiko wa mambo yaliyopingana ibada za nje tu na za shati kabisa teolojia iliyoelekeza kutenda kwa msingi wa nipe nikupe na hakika ya kwamba binadamu anategemea kabisa neema ya Mungu.
Endelea
Kutojali wajibu hata upande wa viongozi wa kanisa na marekebisho safi ya mashirika ya kitawa.
Karne ya 15 ilikuwa kipindi cha umo motomoto wa pekee katika kanisa, ambapo walei wengi zaidi na zaidi walipata aimu nzuri, hivyo walitamani hotuba bora na mafundisho ya kuwasaidia kuishi Kikristo zaidi.
Luther aliitikia haja hizo zilizomgusa sana kama mtu wa wakati wake Luther alitumia kwa nadra neno urekebisho, lakini ukaja kuwa jina la kawaida la matukio yale mengi ya miaka 1517- 1555.
Yaani kuanzia uenezi wa hoja 95 za Martin Luther hadi amani ya Augsburg , kati yake chanzo, yaani mabishano ya kikamisa yaliyosababishwa na teolojia ya Luther, yalichanganyika mapema na sasa.
Uchumi na utamaduni, kutokana na hali halisi ya wakati huo, mbali kuliko mwenyewe alivyofikiri, viongozi mbalimbali wa kaiga mfano wa Luther, ila juhudi zao zikatofautiana.
Ndiyo mwanzo wa madhehebu mengine yanayoitwa ya Kiinjili , jina hilo linataka kusisitiza kwamba yanasimama kwenye msingi wa injili tu, kinyume cha kanisa katoliki liliona mapokeo yake kuwa na umuhimu pamoja na biblia.
Kumbe wafuasi wa Luther na wengineo waliitwa na Wakatoliki "Waprotestanti" maana yake "wapinzani" (to protest=) neno lilianza kutumika tangu wafuasi wa Luther walipopinga azimio la bunge lililotaka Wajerumani wote wasiwe chini ya Papa wa Roma.
Tangu mwaka 1907 tapo la Wapentekoste limeenea duniani kote (linakadiriwa kuwa na waumini milioni karibu 300), na kuathiri madhehebu yote ya zamani (ambapo mara nyingi waumini wa aina hiyo wanaitwa "Wakarismatiki").
KANISA LEO
Kwa miaka 100 ya mwisho asilimia za Wakristo kati ya watu wote zimebaki 33, yaani mmoja kwa watatu, lakini uwiano kati ya mabara umebadilika sana, kwa maana katika Afrika, Asia na nchi nyingine zinazoendelea Wakristo wameongezeka, kumbe Ulaya na Amerika kaskazini wamepungua.
Pew research center inakadiria kwamba mwaka 2050, watazidi bilioni tatu wakati huo Wakatoliki wa Waprotestanti huenda wakalingana kwa idadi.
Kuhusu kuenea ambako Wakristo wanapungua na kwamba kutokana na historia ya kanisa kuwa na mchanganyiko wa mazuri na mabaya, wengine wanahisi kuwa halina maana tena.
INAENDELEA
