Tshisekedi awapiga mkwara wachezaji DR Congo

Baada ya mgogoro uliotokea hivi karibuni kati ya wachezaji wa timu ya taifa ya DR Congo na vilabu vyao, kutokana na kuchelewa kurejea baada ya kusherehekea kufuzu Kombe la Dunia.

Rais wa nchi hiyo, Félix Tshisekedi, ameingilia kati suala hilo na kutoa ujumbe mzito kwa wachezaji:

"Faini zote… zipelekeni kwa shirikisho, sisi tutalipa. Hivyo basi, msibebe mzigo huo.” — maneno ya rais Felix

Kiufupi rais amewahakikishia wachezaji kuwa faini au adhabu yoyote ya kifedha watakayotozwa na vilabu vyao, itagharamiwa na Shirikisho la Soka la Congo.

Lakini pia amewataka wasiwe na wasiwasi na badala yake waweke nguvu zao zote katika kuiwakilisha nchi yao kwa kiwango bora zaidi.

Huu ni uthibitisho wa thamani ya mafanikio yao na furaha waliyoileta kwa taifa zima.


Machapisho maarufu kutoka blogu hii

FIFA yatoa orodha ya vilabu bora duniani, Simba na Yanga zachuana vikali

HISTORIA YA TIMU YA MASHUJAA YA KIGOMA, KUMBE NI SHEA YA JESHI NA WANANCHI

Beno Ngassa mdogo wa Mrisho Ngassa anayekipiga Tanzania Prisons