TRA yaisimamisha Simba SC

TIMU ya Simba SC imetoa sare ya bila mabao na wenyeji, TRA United katika mchezo wa Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara jioni ya leo Uwanja wa Sheikh Amri Abeid Jijini Arusha.

Kwa matokeo hayo, TRA inayofundishwa na Kocha Mrundi, Ettienne Ndayiragijje inafikisha pointi 24 na kupanda kwa nafasi moja hadi ya saba ikiizidi tu wastani wa mabao Dodoma Jiji FC baada ya wote kucheza mechi 18.

Kwa upande wao Simba SC wanafikisha pointi 36 katika mchezo wa 17, ingawa wanabaki nafasi ya pili wakizidiwa pointi nane na mabingwa watetezi, Yanga ambao hata hivyo wamecheza mechi moja zaidi.


Machapisho maarufu kutoka blogu hii

FIFA yatoa orodha ya vilabu bora duniani, Simba na Yanga zachuana vikali

HISTORIA YA TIMU YA MASHUJAA YA KIGOMA, KUMBE NI SHEA YA JESHI NA WANANCHI

Beno Ngassa mdogo wa Mrisho Ngassa anayekipiga Tanzania Prisons