Timua timua ya makocha, yaing' arisha Singida Black Stars, yaipiga KMC
Timu ya Singida Black Stars imeutumia vema uwanja wake wa Airtel Complex uliopo mkoani Singida kufuatia ushindi wa bao 1-0 dhidi ya KMC FC ya jijini Dar es Salaam.
Bao pekee la Singida Black Stars limefungwa na Lamine Jarjou, dakika ya 08 kipindi cha kwanza, kwa matokeo hayo Singida Black Stars imefikisha pointi 28 na mechi 17 ikisogea nafasi moja kutoka ya sita mpaka ya tano ikiishusha Pamba Jiji ambayo jioni inacheza na Yanga SC.
